Featured Kitaifa

WAMILIKI MITANDAO YA KIJAMII WAPEWA ELIMU YA KODI

Written by mzalendo

 

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Na.Alex Sonna na Okuly Julius -MOROGORO

WAMILIKI  wa Mitandao ya Kijamii wameshauriwa kuwa kielelezo katika kuelimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti halali yenye thamani halisi ya huduma aliyeipata.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

“Mitandao ya Kijamii imekuwa nyenzo kubwa ya kuifikia jamii kwa haraka na kwa ukubwa hivyo niwaombe mtumie fursa hiyo kuielimisha jamii umuhimu wa kudai risiti yenye thamani halali ya huduma uliyeipata,”amesema Mwaipaja

Pia amewataka wanamitandao hao kuisaidia serikali kuwaelimisha jamii kuhusu agenda ya maendeleo ya taifa na miradi inyotekelezwa na serikali kwa ajili ya maslahi ya watanzania ikiwemo miradi ya Kimkakati.

Aidha amewapongeza kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya  kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kuhabarisha Umma juu ya mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara hiyo.

“Wizara inawatambua nyie ni wadau muhimu sana katika kutoa taarifa zetu na mmekuwa mkifanya hivyo siku zote na jamii imekuwa ikipata taarifa kupitia mitando yenu bila kuda chochote kwa hilo niwapongeze sana”ameeleza

Katika hatua nyingine Bw.Mwaipaja amewatoa hofu watanzania kuhusu deni la Taifa kuwa linalipika na ndio maana serikali inaendelea kuaminika na inakopesheka kwa manufaa ya Taifa.

“Ukiona mtu anakopeshwa ujue ameaminika na ndio maana mpaka kuna baadhi ya taasisi za nje ya nchi zinaomba zitukukopeshe ama zifadhili miradi yetu kwa hilo tu jamii iamini kuwa nchi ipo salama na deni la taifa bado ni himilivu linalipika,”amesisitiza Mwaipaja

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kongamano hilo Ndg Mathias Canal ameipongeza wizara ya fedha kwa kuandaa kongamano hilo la siku mbili litakalowakutanisha waandishi wa habari za mitandao na kusema kuwa hiyo itakuwa fursa ya kurahisisha utendaji kazi wao kwa umma.

Canal ameitaka wizara ya fedha kuhakikisha kuwa inatoa ufafanuzi kwa umma kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na umuhimu wa mikopo ili kuondoa sintofahamu kwa jamii kuhusu mikopo ya serikali.

”Umuhimu wa kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2023 ambapo amesema Masharti yaliyokuwemo yalisababisha kuwepo kwa ushiriki hafifu wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa ubia.”amesema Bw.Canal

Aidha amewataka  waandishi hao kutoa taarifa kwa kina katika jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, pamoja na kudai risiti kwa kila bidhaa wanazonunua.

“Hongera sana Mkuu wa Kitengo cha Habari Wizara ya Fedha Ndg Benny Mwaipaja kwa kubuni kongamano hili pia tufikishie salamu za pongezi kwa Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba kwa kukubali kufanyika kwa kongamano hili muhimu kwa wanahabari” Amekaririwa Mhe Dkt Mwigulu

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja,akifafanua jambo  wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja,akisisitiza  jambo  wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akionyesha kijitabu cha mkakati wa mawasiliano wa wizara ya Fedha, wakati akifungua kongamano hilo mjini Morogoro Oktoba 23, 2023.

Mwenyekiti wa kongamano la Wanamitandao ya kijamii Ndg Mathias Canal,akifafanua jambo  wakati wa Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Mwenyekiti wa kongamano la Wanamitandao ya kijamii Ndg Mathias Canal,akizungumza wakati wa Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Katibu wa Kongamano hilo Bi.Hope Sylus,akizungumza wakati wa Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha  Bw. Benny Mwaipaja(hayupo pichani) ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.

Wadau wa Mitandao ya Kijamii, wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Afisa Utawala wa Wizara ya Fedha, Bw. Brighton Ngowo (katikati), kuhusu muundo wa wizara hiyo, wakati wa Kongamano la wadau hao ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, linalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro.

 

About the author

mzalendo