Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,akizungumza mara baada ya kuzindua Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Samia Suluhu Hassan, amekemea vitendo vya utoroshaji madini vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo ambapo amesisitiza watakaobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 21,2023 jijini Dodoma wakati wa halfa ya kuzindua mitambo ya uchorongaji Madini kwa wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
“Huo sio uzalendo wala sio Utanzania, wale wenye tabia hiyo waache kwani viwanda vipo na dhahabu inauzwa kwa bei nzuri. Kama watu wameingia mkataba wawambie kwa hawaruhusiwi.
Ameongeza kuwa: “Kama tukikukamata, waliokamatwa juzi wanafahamu kazi yetu. Tufuate sheria, kanuni na miongozi iliyopo kuhakikisha rasilimali madini zinawanufaisha watu wote.”
Hata hivyo Rais amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogo katika kutoa ajira, kukuza uchumi na kipato ambapo serikali imekuwa ikifanya jitihada kuboresha shughuli za uchimbaji mdogo.
Rais Samia amesema kuwa katika kutekeleza suala hilo kwa vitendo, serikali imeondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wachimbaji wadogo ambao watauza madini katika soko la ndani.
”Serikali imeweka punguzo la asilimia mbili la mrabaha na asilimia moja ya ada ya ukaguzi wa madini lengo likiwa wauze madini katika masoko yaliyopo nchini.”
“Miongoni mwa utekelezaji wake ni kwa wachimbaji wanawake ambao walikuwa na changamoto nyingi ili kuwapa nguvu, niliamua kuwanunulia leseni wachimbaji 300 wanawake wakafanye shughuli zao,” amesisitiza
Rais Dk. Samia amesema kuwa STAMICO imeanzisha vituo vya mfano Lwamgasa, Katente na Itumbi ambapo kutokana na ufanisi wa vituo hivyo limeandaa mpango kupanua vituo hivyo vitoe huduma kwa watu wengi zaidi.
Aidha amesema kuwa vituo vingine vitejengwa vya madini ya chokaa mkoani Tanga na Chumvi mkoani Lindi.
“Wakati wa ziara yangu Lindi nilielezwa moja ya changamoto ya wazalishaji chumvi Lindi na Mtwara ni kukosa soko la uhakika. Sasa changamoto hiyo inaelekea kupatiwa suluhisho na STAMICO kwa kujenga kiwanda cha chumvi na kuanzisha shamba darasa.
Ameongeza kuwa: “Msiwasahahu kianamama wa Singida ambao wamejiajiri katika uzalishaji chumvi, nilielezwa katika eneo hilo hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika hadi sasa na kama likipewa mkazo litaleta ufanisi kwa kuongeza kipato.”
Hata hivyo ameeleza kuwa mitambo iliyozinduliwa leo itakuwa chachu ya ukuaji shughuli za uchimbaji kwani zitapatikana taarifa za uhakika na wachimbaji kuacha uchimbaji wa kubahatisha.
Amesema kuwa mitambo ya uzalishaji mkaa mbadala itakayosambaza maeneo mbalimbali nchini, itakwenda kusaidia mpambano dhidi ya uharibifu wa mazingira.
“Imani yangu uzalishaji utakuwa wa kutosha kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, tumeshuhudia STAMICO likisaini mikataba ya kibiashara na wateja wake. Nitoe rai kwa wadau wengine kuendelea kuliamini shirika.
“Tumejiridhisha pasipo shaka kwamba ubunifu, umakini na uweledi wa uongozi wa shirika unaleta tija ya kutosha,” amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko, amesema kuwa mafaniko katika sekta ya madini ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk. Samia.
Naye Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema ili sekta ya madini endelee kuchangia mchango mkubwa lazima utafiti ufanyike kuboresha kanzi data itakayobaini aina ya madini iliyipo na namna ya kuyachimba.
“Tunatumia fedha nyingi kuagiza mbolea wakati yapo maeneo yenye miamba ya malighafi za kutengenezea mbolea. Tukipata taarifa ni rahisi viwanda vikubwa vya mbolea vikafanya uwekezaji mkubwa kuzalisha mbolea.
Ameongeza kuwa: “Dunia inakwenda katika nishati safi, katika nishati zinazohitaji ni madini ya mkakati na muhimu ambayo yapo nchini, lakini ukubwa na kiwango utabainika kupitia taarifa za miamba. Mahitaji ya madini mkakati kwa sasa ni tani milioni 10, mwaka 2050 mahitaji yatakuwa tani milioni 150.”
Awali Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dk.Venance Mwasse, amesema kuwa mafaniko ya shirika hilo ni matokeo ya mageuzi ambayo shirika liliyafanya ambayo yaliasisiwa na Rais Dk. Samia kupia falsafa ya 4R.
Dk.Mwasse amesema kupitia falsafa hiyo walijikita katika kufanya mageuzi ambayo matokeo yake yameonekana kwani STAMICO linaendelea kutekeleza miradi yake kimkakati.
”Mitambo ambayo imezinduliwa leo ina thamani ya sh. bilioni 9.2 huku uwekezaji ambao shirika limeufanya katika mwaka huu ukiwa na thamani ya sh. bilioni 17.3.”amesema Dk.Mwasse
Hata hivyo ameeleza kuwa mitambo mitano iliyozinduliwa ni sehemu ya mitambo 15 ambayo imenunuliwa na STAMICO itakayokwenda kuinua uchumi wa wachimbaji na taifa kwa ujumla.
”Shirika limeendelea kujipambanua kwa kuhudumia makundi maalum ambapo limewezesha wachimbaji wadogo wenye usikivu hafifu kwa kuwapa vifaa, maeneo ya kuchimba na sasa wanakaribia kupata dhahabu.”amesema Dk.Mwasse
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Lucas Selelii, amesema wataendelea kuhakikisha shirika linaendelea kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), John Joseph Kilangi, amesema wizara hiyo imeingia makubaliano na Taasisi ya Jiolojia Tanzania (GST) kufanya utafiti kubaini aina ya miamba iliyopo Zanzibar yenye uwezekano uwepo wa madini.
”Julai mwaka huu SMZ imeingia mkataba na kampuni kutoka Oman kufanya utafiti wa madini na taarifa zimeanza kuonyesha kwamba Zanzibar kuna madini ambapo baada ya miezi mitatu taarifa rasmi zitatoka kisha serikali itatoa tamko.”amesema Bw.Kilangi
Awali Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) John Bina, ameiomba serikali kuweka msamaha wa kodi kwenye vifaa vya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,akizungumza mara baada ya kuzindua Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) John Bina,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TAWOMA, Semeni Malale ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Foundation For Disabilities Hope (FDH) Michael Salali,,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akizungumza mara baada ya kuzindua Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa Ufunguo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse kwa ajili ya kuwakabidhi Wachimbaji wadogo Mitambo ya kupasua na kusagia mawe crasher kwenye hafla iliyofanyika leo Oktoba 21, 2023 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde mara baada ya kuzindua Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,akikagua Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kuizindua hafla iliyofanyika leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma.
Muonekano wa Mitambo ya Uchorongaji Madini kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) iliyozinduliwa.