Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo tarehe 19/10/2023 amewasili Mkoani Tanga na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo .
Aidha, katika ziara hiyo Dkt.Mollel ameongozana na watalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Afya.
Dkt. Mollel atatembelea Hospitali ta Rufaa Bombo kukagua hali ya utoaji huduma na kisha kufanya kikao na watumishi wote wa Hospitali hiyo.