Featured Kitaifa

WAZIRI DKT. GWAJIMA KWENYE MKUTANO WA MERCKY FOUNDATION INDIA.

Written by mzalendoeditor

WMJJWM Mumbai, India

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ni kati ya viongozi wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Merck Foundation inayoshughulika na masuala ya kijamii, afya na kiuchumi unaofanyika Oktoba 18-19, 2023 jijini Mumbai India.

Lengo la Mkutano huo ni kujadili mikakati na programu kuhusu huduma za kijamii kwa Wanawake zikiwemo afya na elimu kwa watoto wa kike husuan ni kutokomeza unyanyapaa kwa wenye tatizo la ugumba barani Afrika na nchi zinazoendelea.

Kutoka nchini Tanzania, Waziri Dkt. Gwajima atawasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu ushirikiano na Merck Foundation na baadaye atashiriki katika majadiliano yanayolenga kuwainua wanawake kiuchumi, kijamii na kuainisha mikakati inayofanywa na nchi kuhusu kundi makundi maalum wakiwemo wagumba.

Taasisi hiyo inawakutanisha watoa huduma za afya, watunga sera, wasomi, watafiti na vyombo vya Habari vya afya zaidi huku ukifuatiliwa na zaidi ya watu 6000 kutoka nchi 70 zikiwemo Afrika, Asia na nchi nyingine duniani.

About the author

mzalendoeditor