Featured Kitaifa

OFISI MPYA TPA NCHINI ZIMBABWE KURAHISISHA BIASHARA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Uchukuzi, Mhe Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amefungua ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) katika Mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, ikiwa ni hatua ya serikali kukuza biashara baina ya Tanzania na Zimbabwe.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo, leo tarehe 16 Oktoba, 2023 l, Profesa Mbarawa amesema hatua hiyo itaisaidia TPA kutoa huduma kwa wateja wake wa nchini Zimbabwe kwa ukaribu na ufanisi zaidi na pia kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili kupitia bandari ya Dar es salaam.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na Maendeleo ya Miundombinu wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhandisi Joy Makumbe amesema uamuzi wa kufungua ofisi mpya mjini Harare utarahisha ufanyaji biashara na usafirishaji shehena kutoka nchi moja hadi nyingine.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Simon Sirro na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Juma Kijavara



Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Maendeleo ya Miundombinu Nchini Zimbabwe Mhe. Mha. Joy Makumbe (wa pili kushoto ), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Jijini Harare nchini Zimbabwe, tarehe 16 Oktoba, 2023.

Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. Simon Sirro ( kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Juma Kijavara ( kulia).

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Maendeleo ya Miundombinu Nchini Zimbabwe Mhe. Mha. Joy Makumbe (wa pili kushoto ), wakifuraia baada kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Jijini Harare nchini Zimbabwe, tarehe 16 Oktoba, 2023.Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. Simon Sirro ( kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Juma Kijavara ( kulia).




About the author

mzalendoeditor