Featured Kitaifa

WATANZANIA WALIOPO NCHINI ISRAEL KUREJESHWA NYUMBANI

Written by mzalendoeditor

Dodoma, 

Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini  Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa  kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na  maeneo mengine ya karibu. Serikali imefikia uamuzi huo  baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba  mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.  

Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani  wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua  pepe: telaviv@nje.go.tz au simu namba: +972 533 044 978  na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa  6 usiku. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA  MASHARIKI 

About the author

mzalendoeditor