Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWAHIMIZA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakati akipokea Maandamano ya Vijana wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itafanya mapitio ya Sera na mitaala ya elimu katika ngazi zote ikiwa ni jitihada ya kuwawezesha vijana nchini. 

 

Aidha, Rais Samia amesema lengo ni kuleta mageuzi makubwa ili elimu inayotolewa kwa viajana iakisi mazingira na mahitaji ya nchi ya mandeleo na kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuajirika kiurahisi.

 

Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa katika Uwanja wa Kwaraa.

 

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuwa zaidi ya asilimia 95 ya mabadiliko ya tabianchi yanatokana na shughuli za binadamu ambazo zinaathiri misimu ya mvua na kupotea kwa vyanzo vya maji. 

 

Rais Samia pia amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha bei ya gesi inashuka ili kuwahamasisha wananchi wengi zaidi kuacha matumizi ya mkaa ambao unaharibu ikolojia na una madhara kiafya. 

 

Vile vile, Rais Samia amewataka wananchi hususan wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na pwani ya Bahari ya Hindi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El Nino wakati wa msimu wa vuli.

 

Kupitia mbio za Mwenge mwaka huu, jumla ya miradi 1,424 yenye thamani ya shilingi trilioni 5.3 ilishughulikiwa katika Halmashauri 195 nchini na kati ya hiyo miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 ilibainika kuwa na dosari. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakati akiangalia Vijana wa Halaiki walipokuwa wakionesha maumbo mbalimbali uwanjani wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja wa Vyama vya Siasa wakiwa kwenye Sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa Heshima ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivalishwa Skafu na Kijana wa Skauti mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Babati kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.

Wakuu wa Mikoa pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye Sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio hizo katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.

About the author

mzalendoeditor