Featured Kitaifa

ZIJUE MBINU ZA MONTESSORI ZINAZOMSAIDIA MTOTO 

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi wa  Montessori Community of Tanzania (MCT),Bi. Sarah Kiteleja,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki   Kilele Cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kilichoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfumo wa Ramani wa kidijitali wa utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkurugenzi wa  Montessori Community of Tanzania (MCT),Bi. Sarah Kiteleja amesema mbinu za ufundishaji za Montessori zinamwandaa mtoto  kuwa na ujasiri na uwezo wa kujitegemea pamoja na kuishi katika mazingira yoyote.
Bi.Sarah ameyasema hayo leo Oktoba 5,2023  Jijini Dodoma wakati wa  Kilele Cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lililoenda   sambamba na Uzinduzi wa Mfumo wa Ramani wa kidijitali wa utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini.
Bi.Sarah amesema wanafanya kazi kwa karibu na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Maendeleo ya Jamii kutatua changamoto ya Kusoma,Kuandika na Kuhesabu.
Amesema kupitia vifaa vya Montessori  wameanza kufundisha mtoto kusoma,kuandika na kuhesabu.
Amesema kwenye hesabu wanafundisha msingi wa hesabu na kumwelewesha mtoto kwa kugawanya,kujumlisha na kuzidisha na kufanya hesabu mpaka 1999.
Amesema kupitia mfumo huo unamsaidia mtoto kuwa na ujasiri uwezo wa kujitegemea,kuishi mahali popote katika mazingira yoyote.
“Montessori inampatia mtoto life skills ambazo zitamsaidia kuishi popote,”amesema Bi.Sarah
Amesema wameweza kufanya utafiti kuangalia mbinu hiyo ya ufundishaji na imeleta faida gani katika Jamii.
“Katika utafiti huu imeonekana kwamba Montessori inaibua vipaji kuweza kuwa na ujuzi na kujiamini na uwezo wa kufanya vitu vipya,” amesema 
Hata hivyo amesema mipango ya Shirika ni kuanza kufundisha walimu wa shule za msingi katika Chuo cha Mwanza ambapo kozi inatarajia kuanza Januari mwakani.
“Lakini pia mipango mingine tumeanza utafiti katika Mkoa wa Bukoba kwa ajili ya kuwafundisha walimu wa Serikali ili waweze kuyamudi madarasa yao”amesema Bi.Sarah
Pia amesema wana  vyuo 7 vya Montessori na tumefanikiwa kufundisha zaidi ya walezi 5000 na kuanzisha vituo vya malezi 2500 nchi nzima.
Amesema kupitia vituo vya malezi wamefanikiwa kufundisha watoto zaidi ya 100,000.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Philip Mpango,akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa  Montessori Community of Tanzania (MCT),Bi. Sarah Kiteleja mara baada ya kutembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Kilele Cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kilichoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfumo wa Ramani wa kidijitali wa utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa  Montessori Community of Tanzania (MCT),Bi. Sarah Kiteleja,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki   Kilele Cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kilichoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfumo wa Ramani wa kidijitali wa utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor