Featured Kitaifa

WATOTO ZAIDI 2800 MIKOA YA DODOMA NA SHINYANGA WAFIKIWA NA MRADI ELIMU JUMUISHI SHULE ZA MSINGI

Written by mzalendoeditor

Afisa Kutoka  Shirika Slisilo la kiserikali la Tanzania Chesire Foundation Anna Nguse,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo wakati  wiki ya maonyesho ya  mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) kuelekea Mkutano Mkuu wa Mashirika hayo yanayoendelea katika viwanja vya Jakay Kikwete vilivyopo jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Chesire Foundation,limefanikiwa kuwafikia watoto zaidi ya 2800 kutoka katika mikoa ya Dodoma na Shinyanga katika utekelezaji wa mradi wa elimu jumuishi
katika shule za msingi.

Hayo yamesemwa  leo Oktoba 3,2023 na Afisa Kutoka Tanzania Chesire Foundation Anna Nguse katika maonyesho ya wiki ya taasisi zisizo za kuserikali yanayoendelea katika viwanja vya Jakay Kikwete vilivyopo jijini Dodoma.

Nguse alisema lengo la mradi Jumuishi katika mikoa hiyo ni pamoja na kuwainua watu wenye ulemavu kielimu na kiuchumi, lakini pia kuwasaidia kutotengwa na jamii nyungune.

“,Mradi wa elimu Jumuishi katika mikoa hiyo,umesaidia kwa kiasi kikubwa, kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu wakiwa wamechangamana na watoto wa kawaida, na hii imesaidia jamii hiyo
kujiona sawa na wengine,”alisema Nguse.

Nguse amesema kwa upande wa shinyanga mradi wa elimu Jumuishi unatekelezwa katika shule za msingi 47 ambapo umeonyesha mafanikio makubwa kutokana na mwitikio ulioonyeshwa na wazazi kwa kuwaleta watoto katika shuke kupata elimu.

Nguse alisema wito wake kwa serikali ni pamoja na kuwataka kuendelea kuisisitiza jamii kuhakikisha inawapeleka watoto wenye ulemavu shuleni kwa ajili ya kupata elimu.

Anasema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pamoja na watu kuwa na uwelewa mdogo ya kuwa hata watu wenye ulemavu wanahaki ya kusoma kama ilivyo jamii nyingine.

Naye Enock Isaya mmoja wa wanufaika wa mradi wa elimu Jumuishi  amesema kuwa hakuna sababu ya kuwaficha watoto wenye ulemavu,badala yake wawatoe ili waende kupata elimu jumuishi, kwa sababu serikali hivi sasa imewekeza kwenye elimu, ikiwemo kuongeza bajeti.

Naye Mwita Marwa amesema mradi wa elimu jumuishi una umuhimu mkubwa hivyo wazazi wanapaswa kutoa Ushirikiano pale watoto wenye ulemavu wanapotakiwa kwenda shuleni, wawapeleke.

Afisa Kutoka  Shirika Slisilo la kiserikali la Tanzania Chesire Foundation Anna Nguse,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo wakati  wiki ya maonyesho ya  mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) kuelekea Mkutano Mkuu wa Mashirika hayo yanayoendelea katika viwanja vya Jakay Kikwete vilivyopo jijini Dodoma.

Mnufaika wa mradi Bw.Mwita Marwa,akizungumza wakati  wiki ya maonyesho ya  mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) kuelekea Mkutano Mkuu wa Mashirika hayo yanayoendelea katika viwanja vya Jakay Kikwete vilivyopo jijini Dodom

Enock Isaya mmoja wa wanufaika wa mradi wa elimu Jumuishi ,akielezea alivyonufaika na mradi huo.

About the author

mzalendoeditor