Featured Michezo

KONDWANI CHIBONI AIPELEKA SIMBA SC MAKUNDI CAFCL

Written by mzalendoeditor

Bao la kujifunga beki wa Power Dynamos Kondwani Chiboni dakika ya 68 limeipeleka Timu8 ya Simba SC kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji wao  Andy Boyeli dakika ya 16 akifunga bao kwa shuti lililomshinda kipa wa Simba SC.

Kipindi cha pili Simba SC waliwapelekea moto Power Dynamos na mnamo dakika ya 68 Kondwani Chiboni alijifunga baada ya John Bocco kuisumbua ngome ya wageni.

Kwa matokeo hayo Simba SC wametinga hatua ya makundi kwa mabao ya ugenini ambayo mechi ya  kwanza Simba SC walitoka sare ya mabao 2-2 hivyo jumla kuwa 3-3 na Simba kufaidika na mabao ya ugenini.

About the author

mzalendoeditor