Featured Kitaifa

MRADI WA HEET MZUMBE WATOA BAJAJI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU

Written by mzalendoeditor

Mratibu wa mradi Higher Education for Economic Transformation (HEET) Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Eliza Mwakasangula akieleza kuhusu shughuli zinazofanywa na Mradi wa HEET, katika eneo la Elimu Jumuishi  (Mahitaji Maalumu). Katika hafla hiyo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi amekabidhi hati ya makubaliano ya umiliki wa bajaji kwa Bw. Revocatus Butawantemi (Mtumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe) ili iweze kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake. Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 29.9.2023 katika Kampasi Kuu Mzumbe.

Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET Dkt. Hawa Tundui, akifafanua jambo kwa Bw. Revocatus Butawantemi kuhusu miongozo na taratibu za matumizi ya Bajaji kwa mujibu wa utaratibu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Bajaji hiyo imetolewa na Mradi wa HEET kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya mtumishi huyo mwenye mahitaji maalumu.

Dkt. Editha Ndunguru, Mratibu wa Mradi wa HEET (Kitengo cha Mazingira) akielezea kazi za eneo la mahitaji Jumuishi katika Mradi wa HEET wakati wa hafla ya kukabidhi bajaji kwa Bw. Revocatus Butawanteni. 

Mratibu wa mradi HEET Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Eliza Mwakasangula akikabidhi Hati ya makubaliano ya msaada wa Bajaji kwa Prof. Allen Mushi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala. Bajaji hiyo imekabidhiwa leo tarehe 29.9.2023 kutoka Mradi wa HEET.

Prof. Allen Mushi, Naibu Makamu Mkuu wa chuo, Mipango Fedha na Utawala akimkabidhi Ndugu Revocatus Butawantemi (Mtumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe), hati ya makubaliano ya umiliki wa Bajaji iliyotolewa na mradi wa HEET ili kumwezesha kutekeleza majukumu yake. Makabidhiano hayo yamefayika leo 29.9.2023 katika Kampasi Kuu, Chuo Kikuu Mzumbe.

Pichani Bw. Revocatus Butawantemi mara baada ya kukabidhiwa Bajaji na Mratibu wa HEET Dkt. Eliza Mwakasangula pamoja na  Prof. Allen Mushi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala. Bajaji hiyo imetolewa mradi wa HEET

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miliki Mhandisi Wolta Shiyo, akitoa neno la shukrani kwa timu ya HEET pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa msaada wa Bajaji itakayo msaidia Bw. Revocatus Butawantemi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja  na waratibu wa Mradi wa HEET baada ya kumkabidhi Ndugu Revocatus Butawantemi Bajaji mapema.

About the author

mzalendoeditor