Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 29,2023 wakati akizindua mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyijka Disemba3 Mwaka huu Jijini Dodoma zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Katibu Mtendaji wa Sepesha rushwa,Kubega Dominic,akitoa taarifa kuhusu mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyijka Disemba3 Mwaka huu Jijini Dodoma zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Katibu wa Chama cha riadha Mkoa wa Dodoma Bw.Robert Mabonye,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyijka Disemba3 Mwaka huu Jijini Dodoma zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyijka Disemba3 Mwaka huu Jijini Dodoma zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri ametaka wale watakao pata zabuni ya kujenga Viwanja vya michezo kwaajili ya mashindano ya AFCON kujiepusa na vitendo vya rushwa kwani athari zake ni nyingi kwa jamii.
Shekimweri ameyaeleza hayo leo Septemba 29,2023 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyijka Disemba3 Mwaka huu zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Amesema ni muhimu kutekelza adhma ya Rais katika kumpa heshima ambayo amepewa kuwa mwenywji wa mashindano hayo kwakuepukana na Vitendo hivyo ambavyo havina tija kwa maendeleo ya Taifa.
“Tusipozingatia kanuni na uadilifu katika utendaji kazi na tunaweza kusababisha kuwa na Wataalam qasio na sifa na kuleta hasara kwa Taifa,”
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha riadha Mkoa wa Dodoma Bw.Robert Mabonye amepongeza ujio wa mbio hizo za sepesha rushwa Marathon kwani ni fursa kwa wakazi wa Dodoma na Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki.
“Ni muhimu kwa wana Dodoma Sasa na Watanzania kujitokeza Kushiriki kwani baadae kutakuwa na zawadi mbalimbali,”
Awali Katibu Mtendaji wa Sepesha rushwa,Kubega Dominic amesema Sepesha rushwa Marathon ni mbio zinazoandaliwa na vijana wa kupinga rushwa huku akieleza malengo mbalimbali..