Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujitambulisha, kujifunza , Kukagua Miradi inayotekelezwa na kujionea shughuli zinazosimamiwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye ofisi za Shirika Hilo na kutembelea Kituo Cha Kuratibu Shughuli za Utafutaji na Uokoaji Majini (MRCC) vyote vilivyopo Jijini Dar es Salaam Tarehe 27 Septemba, 2023 |
Na Mwandishi wetu Dar es Salaama
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe David Kihenzile amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) kwa usimamizi na udhibiti makini wa vyombo vinavyotumia usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa haraka wa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau hao hivyo kuwahakikishia usalama
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe David Kahenzile wakati wa ziara ya kutembelea, kujifunza, kujitambulisha na kukagua ofisi za tasac na miradi mbalimbali ya udhibiti na usimamizi wa vyombo vya usafiri Nchini kikiwemo kituo cha Kuratibu shughuli za Utafutaji na Uokoaji Majini vyote vilivyopo Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Septemba,2023
“ Serikali inaridhishwa na ubunifu na jitahada zinazofanywa na mamlaka hii yenye jukumu la kudhibiti huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji nchini ikiwemo kufanya ukaguzi wa meli za nje zinazoingia nchini,kudhibiti vivuko,utunzaji mazingira na kuratibu kazi za utafutaji na uokoaji ambapo sasa vituo vinajengwa kwenye bahari zetu na maziwa yote” amesisitiza Kihenzile
Mhe Kihenzile amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miradi ya kimkakati nchini ikiwemo upanuzi wa bandari zetu,ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo pia kuendelea kutafuta wadau binafsi wa kushirikiana nao kuziendesha hali itakayosababisha ujio wa meli zaidi Nchini na kuwahakikishia wadau Maji ya Tanzania yako salama.
“nimepata fursa pia ya kutembelea kituo cha kuratibu Shughuli za uokoaji na utafutaji majini,vituo hivi vinajengwa nchi nzima kwenye bahari zetu na maziwa hivyo niwahakikishie wadau na watumiaji wa vyombo vya usafiri majini, maji ya Tanzania yako salama, bahari zetu na maziwa yetu ni salama katika usafirishaji kwa njia ya maji tumieni fursa hii kuwekeza zaidi kwenye njia hii ya usafirishaji kwani ni rahisi, salama na ya gharama nafuu” amesisitiza Kihenzile
Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) Bw. Nelson Mlali amesesma TASAC ilianzishwa tarehe 23 februari,2018 chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania ikiwa na majukumu ya kufanya kazi za uwakala wa forodha,kusimamia usalama na ulinzi wa usafiri majini na kudhibiti huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji nchini.
“mbali na jukumu la kusimamia na kudhibiti usafiri majini Shirika pia lina jukumu la kipekee la kutoa huduma za uwakala wa forodha kwa mujibu wa kifungu cha saba na shehena zinazohudumiwa na TASAC ni pamoja na silaha na vilipuzi,makinikia,kemikali za madini,nyara za Serikali na wanyama hai” amesisitiza Mlali
Kwa upande wa mafanikia Bw Mlali amesema Shirika limefanikiwa kufungua ofisi 16 katika maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma kwa wananchi, kuongea idadi ya uhudumiaji wa kadhia kutoka 6,000 mwaka 2019/20 mpaka zaidi ya kadhia 10,000 mwaka 2021/22,kuongeza idadi ya watoa huduma zinazodhibitiwa ambapo idadi ya leseni na vyeti vya usajili ilifikia 1,278 mwaka 2020/22 ukilinganisha na vyeti 941 mwaka 2018/19 pia Shirika limefanikiwa kupata Hati safi za ukaguzi wa Hesabu kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuanzia mwaka 2018/19 mpaka 2020/21 licha ya changamoto chache zilizopo.
Akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi Afisa kwenye kituo cha kuratibu Shughuli za utafutaji na Uokoaji MajinI(MRCC) Bw. Emmanuel Lusuva amesema majukumu ya kuratibu wa shughuli za Utafutaji na Uokoaj majinii,kubadilishana taarifa zinazohusiana na uharamia na shughuli zisizo rasmi majini,kupokea taarifa za uchafuzi mazingira,kufuatilia mienendo ya meli zilizosajiliwa Nchini na kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wadau wa usafiri majini wakiwemo wavuvi wadogo wadogo