Featured Michezo

HAFLA YA MAKABIDHIANO YA TAASISI YA HAKI MILIKI YAFANYIKA ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akisisitiza jambo wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Saidi Shaabani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita (kushoto)akimkabidhi Waraka wa Makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Saidi Shaabani  katika hafla ya makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki  iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.

Balozi wa Haki miliki Afrika Salum Stika akitoa nasaha kwa niaba ya Wasanii katika hafla ya makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Hakimiliki kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita (katikati)akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Saidi Shaabani wakiwa katika Picha ya pamoja na Wasanii na Viongozi mbalimbali baada ya kumalizika zoezi la  makabidhiano ya Taasisi ya Msajili waHaki miliki  kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda hafla iliofanyika katika    Ukumbi wa Wizara ya Habari Migombani Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR,27/09/2023.

Na Maelezo Zanzibar     

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imesema itawajengea uwezo mameneja wanaosimamia kazi za wasanii ili msanii auzwe kibiashara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban wakati wa makabidhiano ya Taasisi ya Msajili wa Haki miliki Cosoza baina ya Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo na Wizara hiyo huko Migombani Mjini Unguja. 

Amesema uwezo huo utawasaidia wasimamizi hao na wale wanaopenda kazi hiyo kuwafunza jinsi ya kuwasimamia na njia watakazozitumia katika kujenga hadhi ya wasanii hao.

Amesema Wasanii duniani wanaingiza fedha kutokana na kuwepo watu madhubuti wanaosimamia kwa kuwatafutia fursa katika kuuza kazi zao. 

Aidha Waziri huyo amesema msanii aliyekua hana mtu wa kumsimamia atakuwa anayumba kutokana na kufanya kazi zote mbili kwa wakati mmoja, ikiwemo ya kutunga kazi yake na kutafuta fursa ya kupata pesa kupitia kazi yake ya sanaa.

Sambamba na hayo ameahidi kuendeleza gurudumu hilo na amemtaka Waziri wa Habari kushirikiana katika kusimamia haki za wasanii na maslahi ya kibiashara.

Waziri Tabia amesema ni lazima kufanyiwa kazi suala la wasanii hasa chipukizi kuchukuwa kazi zao na wasanii wa zamani na kuzipiga katika shughuli mbalimbali.

Amsema wasanii hao wamekuwa wakipiga nyimbo  bila ya ridhaa kutoka kwa wasanii wenyewe jambo amablo ni kinyume na sheria.

Amefahamisha kuwa anachotaka ni kuona wasanii wanaubunifu wao na kuwa kazi zao mpya bila ya kuiga kutoka kwa wasanii wengine ili mtu aweze kufaidika na alichokitunga.

Nae Muwakilishi wa wasanii na wabunifu Salum Stika amepongeza kwa hatua hiyo ambayo itasaidia tasnia yao kugeuka kuwa biashara kwa kuongeza mapato kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

About the author

mzalendoeditor