Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ya Dar es Salaam, Eneo la Ujenzi wa Matenki ya Kuhifadhia Mafuta, Ujenzi wa mashine ya upimaji wa kiwango Cha mafuta yanayoingia Nchini(Flow Meter) na Bandari Kavu ya Kuhifadhia Makasha vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) , vyote vilivyopo Kigamboni sambamba na ukaguaji wa Gari Namba Zero mpaka Namba Kumi na Moja za Bandari ya Dar es Salaam Jijini humo ,Tarehe 26 Septemba, 2023 |
Na Mwandishi wetu Dar es Salaama
Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ina mpango wa kujenga matanki makubwa ya kuhifadhia mafuta(farm tank) yatakayokuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 360,000 eneo la kigamboni jijini dar es salaam
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe David Kahenzile wakati wa muendelezo wa ziara ya kutembelea, kujifunza, kujitambulisha na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini(TPA) ya uboreshaji wa miundombinu ya Bandari nchini kwa Bandari ya Dar es salaam, Jijini humo tarehe 26 Septemba,2023
“ Serikali ya awamu ya sita imeamua kujenga matanki ya kuhifadhia mafuta eneo la Kigamboni yatakayokuwa na uwezo wa kuhifadhi tani laki tatu na elfu sitini kwani kuna changamoto kubwa meli za mafuta zikitoka huko inabidi zisubiri mpaka meli moja ishushe ndiyo iingie hili tunakwenda kulipunguza kama si kulimaliza kabisa ili kuongeza ufanisi wa bandari yetu ya dar es salaam”
Mhe kihenzile amesema utaratibu huu wa kujenga matanki makubwa ya kuhifadhia mafuta ambao serikali imebuni na ambao ipo katika hatua za kumpata mkandarasi utaondoa kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta Nchini ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na kuleta usumbufu kwa wananchi
“kwa utaratibu huu mafuta yatakuwa yanahifadhiwa halafu watu wengine au Nchi zingine wanakuja kuchukulia hapa Kigamboni kwa kiwango cha juu zaidi na hii itaondoa adha ya upatikanaji wa mafuta nchini, tutasafirisha kwa wingi kwenda nchi jirani lengo ni kuboresha ufanisi wa Bandari zetu hasa bandari ya Dar es salaam” amesisitiza Kihenzile
Katika ziara hiyo Mhe Kihenzile pia alipata fursa ya kutembelea eneo la upimaji wa kiwango cha mafuta yanayoingia Nchini na mahali itakapojengwa mashine mpya ya upimaji wa kiwango cha mafuta (flow meters) lililopo kigamboni ambapo utajengwa mtambo mkubwa zaidi na kutembelea Gati zote kuanzia gati namba Zero mpaka 11 za bandari ya Dar es salaam na eneo la ekari 23 itakapojengwa yadi ya kuhifadhia makasha,magari ,ofisi za mamlaka, na cold room lililokuwa likimilikiwa na EPZA na sasa limekabidhiwa TPA
Akitoa maelezo ya mradi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini Mha Juma Kijavara amesesma eneo hilo la Kigamboni ambapo utatekelezwa mradi mkubwa wa ujenzi wa Matanki ya kuhifadhia mafuta ya tani laki tatu na elfu sitini lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Fedha na tayari Wizara hiyo imeshalikabidhi wa Mamlaka ya Usimamizi Nchini (TPA) na sasa utaratibu wa kumpata mkandarasi unaendedlea na atakapopatikana ujenzi wake utachukua miaka minne hadi kukamilika.
Akizungumzia changamoto za uhifadhi na uondoshwaji wa mizigo kwa bandari kavu za kigamboni na ubungo, Meneja wa Bandari ya Dar es salaam Bw. Mrisho Mrisho amesema changamoto inayowakabili madereva wa malori wanaotegemewa kuondosha mizigo kwa haraka zaidi ni tozo kutoka halmashauri za manispaa zao zinazosababisha madereva kwa kukwepa tozo kupaki hovyo barabarani na kusababisha msongamano ambao hupunguza ufanisi wakati Tayari Bandari inalipa Service levy kwa manispaa zote