Featured Kitaifa

CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM CHAINGIA MAKUBALIANO NA CHUO CHA KOREA KUSINI.

Written by mzalendoeditor
Balozi wa Korea ya Kusini Kim Yong Jung akiwa na Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Capt. Adrew Matilya akishuhudia utiaji Saini wa Makubaliano ya Mafunzo kati ya chuo Bahari ya Dar es Salaam (DMI) na chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT), Makubaliano hayo yameingiwa kati ya Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo na Mwakilishi wa chuo cha KIMFT Dkt. Min Jung. Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa chuo cha Baharia Dar es Salaam (DMI) Dkt Tumaini Gurumo na Mwakilishi wa Chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT) Dkt. Min Jung (kulia) wakionyesha nyalaka ya Mkutaba wa Makubaliano walioyaingia katika vyuo hivyo katika kubadilisha uzowefu.

 

Na Mwandishi wetu Dar es Salaama 
 
Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaama (DMI) Dkt Tumaini Gurumo amesema chuo hicho kimeingia makubaliano ya miaka mitano ya kubadilishana uzoefu wa elimu ya Ubaharia na Ujenzi wa Meli na Chuo cha Korea Institute of Maritime and Fisheries Technology ambayo yatawezesha kunufaisha pande zote mbili za vyuo hivyo kwa walimu na wanafunzi .
 
Dkt. Gurumo amesema kuwa makubaliano hayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo cha DMI kwa ujumla. “Chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT) kimeendelea kwa Teknologya ya Ujenzi wa Meli na Elimu ya Ubaharia na wana vifaa vya kisasa hivyo ni muhimu sana kwa chuo cha DMI kupata nafasi hiyo muhimu ya kushirikiana na chuo hicho” Alisema Dr. Gurumo.
 
Gurumo alisema kuwa makuabaliano hayo yatawezesha wanafunzi wa chuo DMI kwenda chuo cha KIMFT nchini korea kujifunza elimu ya Vitendo ili wanafunzi hao waendandane na soko la Dunia pamoja na wanafunzi kutoka KIMFT ili kuja kujifunza DMI kuhusu Elimu inayotolewa katika chuo cha DMI.
 
Kwa upande wake Balozi wa Korea nchini Tanzania Ndugu Kim Yong Jung amesema kuwa makuabaliano hayo yana manufaa makubwa na yatawezesha wanafunzi wa DMI kwenda nchini Korea kupata mafunzo muhimu ya vitendo katika chuo kikubwa na Teknologia ya hali ya juu.
 
Naye Mwakilishi wa chuo cha KIMFT Dr. Min Jung amesema kuwa anayofuraha kwa kuingia makubaliano na chuo cha DMI kwani wanafunzi na walimu watapata uzoefu mkubwa katika kuhudumia Meli na maswala yote ya ubaharia .
 
“ KIMFT ni chuo cha kwanza kwenye Teknologia na Ujenzi wa Meli katika nchi ya Korea, hivyo naamini chuo cha DMI kitapata uzoefu Mkubwa kwa wanafunzi na walimu kwenda Korea kujifunza” Alisama Dkt. Jung
 
Makubaliano hayo yameingiwa katika chuo cha DMI jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Korea nchini Tanzania pamoja na viongozi wa chuo cha KIMFT na Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya DMI , Uongozi wa Chuo cha DMI na Wanafunzi walihudhuria.

 

About the author

mzalendoeditor