Featured Kitaifa

BROTHERHOOD SURVEY SERVICES CO. LTD , WADAU WACHANGIA MABATI UJENZI WA BWENI KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUHANGIJA

Written by mzalendoeditor
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakikabidhi moja kati ya mabati 60 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la wavulana katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited ya Mjini Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Mjini Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali huku wakichangia mabati 60 yenye thamani ya shilingi Milioni 2.6 ili kukamilisha ujenzi wa bweni katika kituo hicho.

 
Akizungumza katika kituo hicho leo Jumamosi Septemba 23,2023 Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu amesema wamefika katika kituo hicho kutokana na kwamba wanajali watoto na kama sehemu ya jamii wana wajibu wa kujali ustawi wa jamii na watoto.
 
 
“Brotherhood Survey Services Company Limited kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Kampuni ya Angel Soap, Gven Wear & Wedding, Oval Technologies, Sarah Sanula, Dotto Sikawa na Glory Mbia wa WFT tumefika hapa katika kituo cha Buhangija na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni na juisi lakini kubwa zaidi tumechangia mabati 60 yenye thamani ya shilingi 2,625,000/= ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana katika kituo hiki”,ameeleza Bulugu.
“Tumeambiwa ili kukamilisha ujenzi huu panahitajika mbao pamoja na mabati 240, nasi Brotherhood Survey Services Co. Ltd kwa kushirikiana na wadau wengine tumechangia mabati haya 60 kama chachu ya kuwaamsha wengine wenye nafasi wajitokeze kusaidia ujenzi wa bweni hili hasa tukikumbuka mwaka jana tulipatwa janga la bweni kuungua katika kituo hiki ili kuunga mkono juhudi za serikali”,ameongeza Bulugu.
 
Mwalimu wa Malezi katika kituo cha Buhangija, Mashinde Daudi Elias ameishukuru Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau kwa msaada waliotoa katika kituo hicho huku akieleza kuwa hivi jumla ya watoto waliopo katika kituo hicho ni 194 (watoto wenye ualbino, viziwi na wasioona).
 
Nao wanafunzi wa kituo hicho wameshukuru kupatiwa msaada huo na wamewaomba wadau kuendelea kuwatembelea kwani wanapata faraja wanapopata wageni.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakitembelea bweni la wavulana linaloendelea kujengwa katika kituo cha Buhangija.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles amesema Kampuni yao inajihusisha na Uendelezaji wa ardhi, ushauri kuhusu masuala ya ardhi, usimamizi wa mali yakiwemo majengo, magari na viwanja, ukusanyaji wa ushuru na mikopo, udalali, uchoraji wa ramani za majengo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.
 
 
“Brotherhood Survey Services Company Limited kwa sasa tuna mradi mpya wa viwanja vya makazi na biashara uitwao Oysterbay Project ambao upo kilomita 4 tu kutoka katikati ya Manispaa ya Shinyanga, eneo hili lipo barabarani kabisa kwenye lami uelekeo wa Old-Shinyanga palipo na kona ya Chibe”,amesema Charles.
 
Amesema mradi wote umeshawekewa barabara pamoja na beacons na kusogezewa maji kwa kila kiwanja ambapo huduma za kibinadamu kama umeme, shule, zahanati na eneo la kuchezea watoto na vingine vingi, vyote vinapatikana na kwamba viwanja vinauzwa kuanzia shilingi Milioni 2.5.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Septemba 23,2023 – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija Manispaa ya Shinyanga
Mwalimu wa Malezi katika kituo cha Buhangija, Mashinde Daudi Elias akitoa neno la shukuruni kwa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau kwa msaada waliotoa katika kituo hicho
Mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija akiishukuru Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau kwa msaada waliotoa katika kituo hicho
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakikabidhi moja kati ya mabati 60 yenye thamani ya shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la wavulana katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu za zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau kwa watotot wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Muonekano wa sehemu za zawadi (Angel Soap) zilizotolewa kwa watotot wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd, wanafunzi na wadau wakiwa wameshika Sabuni za unga zinazotengenezwa na Kampuni ya Angel Soap ya Mjini Shinyanga
Wafanyakazi wa Kampuni ya Angel Soap ya Mjini Shinyanga wakigawa sabuni kwa watoto 
Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles akigawa sabuni kwa watoto 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakigawa juisi na soda kwa watoto 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakigawa juisi na soda kwa watoto 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakigawa juisi na soda kwa watoto 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd na wadau wakitembelea bweni la wavulana linaloendelea kujengwa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga ambapo wamechangia mabati 60 yenye thamani ya shilingi Milioni 2.6
Muonekano wa bweni la wavulana linaloendelea kujengwa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

About the author

mzalendoeditor