MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeendelea kung’ang’ania Kileleni Mwa Msimamo baada ya kuichapa bao 1-0 Timu ya Namungo Mchezo uliopigwa uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Bao la Yanga SC limefungwa dakika ya 88 na Kiungo Mkabaji Mudathir Yahya akimalizia pasi ya Yao.
Kwa ushindi Yanga imefikisha Pointi 9 huku ikiwa imecheza mechi tatu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa Mechi mbili majira ya saa kumi jioni Simba SC itashuka uwanja wa Uhuru kucheza na Coastal Union na mchezo wa pili Azam FC wataikaribisha Singida Big Star uwanja wa Chamazi Complex.