Featured Kitaifa

MABEHEWA YA SGR KUKAMILIKA KWA WAKATI KOREA

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Majaribio Dongjin Son, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni ya mwendo kasi, ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea kiwanda hicho Changwon, Korea Kusini. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akipewa maelezo na Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Majaribio wa Kampuni ya Hyundai Rotam, Dongjin Son, pamoja na kutazama hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mabehewa, wakati ujumbe wa Tanzania ulipotembelea kiwanda hicho Changwon, Korea Kusini.

Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa moja ya kichwa cha treni, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni ya Hyundai Rotam, Kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni Changwon, Korea Kusini.

Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa moja ya kichwa cha treni wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni ya Hyundai Rotam, kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni Changwon, Korea Kusini.

Muonekano wa moja ya behewa linaloendelea kutengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea kampuni hiyo kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini.

Muonekano wa ndani wa moja ya behewa linaloendelea kutengenezwa katika kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni hiyo kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara hiyo na viongozi wa Kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe wa Tanzania ulipotembelea kampuni hiyo, kuona maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini. Kulia kwake ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje. Bw. Melckzedeck Mbise, Kamishna Idara ya Fedha za Nje Bw. Rished Bade na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Nuru Ndile.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Korea Kusini)

Na. Saidina Msangi, WF, Busan, Korea Kusini

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, na Treni ya mwendokasi vinavyotengenezwa na kampuni za Hyundai Rotem na Sing Sung Rolling Stock Technology (SSRST) za Korea Kusini.

Alisema hayo mara baada ya kutembelea kampuni hizo zilizopo katika mji wa Changwon, Korea ya Kusini, zilizoingia mkataba na Serikali ya Tanzania, wa kutengeneza mabehewa 59 na vichwa vya treni 17 pamoja treni za Mwendokasi (Electric Multiple Unit) 10.

‘‘Kwa kampuni zote mbili maendeleo ni mazuri kwa hatua iliyofikiwa na wametueleza kuwa wanatarajia kukamilisha utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni kama ilivyoainishwa katika makubaliano, na kwa kweli tuliyoyaona yako katika hali nzuri’’alisema Bi. Amina.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa sekta husika kuhakikisha kuwa inatoa mafunzo kwa watakao husika na kuendesha, kuhudumia treni hizo wanajengewa uwezo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma bora kwa uendelevu.

‘‘Tunashauri wenzetu watakaosimamia uendeshaji wa treni hizi kwa Tanzania wajengewe uwezo wa uendeshaji na utunzaji ili mabehewa na vichwa viendelee kuwa na ubora huu kwa ajili ya huduma na pia yaweze kudumu kwa muda mrefu’’, alisisitiza Bi. Amina.

Ujumbe wa Tanzania ulikuwa Busan Korea ya Kusini kuhudhuria mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini ambapo Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika mkutano huo.

About the author

mzalendoeditor