Rais Mstaafu Dkt. Jakata Mrisho Kikwete akiwa na Mheshimiwa Ellen Johnson Sirleaf, Rais Mstaafu wa Liberia (kati) na Mheshimiwa Michelle Bachelet, Rais Mstaafu wa Chile wakiwa tayari kutoa mafunzo maalumu kwa mawaziri kutoka mataifa mbalimbali yanayoendelea katika Mpango wa Uongozi wa Harvard (Harvard Ministerial Leadership Program) inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard jijini Boston, Marekani.
Rais Mstaafu Dkt. Jakata Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanoshiriki kutoa mafunzo hayo. Katikati ni Mheshimiwa Ellen Johnson Sirleaf, Rais Mstaafu wa Liberia, wa pili kushoto ni Mheshimiwa Michelle Bachelet, Rais Mstaafu wa Chile; Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia na kushoto ni mwenyeji wao wakiwa tayari kutoa mafunzo maalumu kwa mawaziri kutoka mataifa mbalimbali yanayoendelea katika Mpango wa Uongozi wa Harvard (Harvard Ministerial Leadership Program) inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard jijini Boston, Marekani.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa jijini Boston, Marekani, katika picha ya pamoja ya viongozi wastaafu na Mawaziri wa Afya na Elimu kutoka mataifa mbalimbali yanayoendelea wanaohudhiria mafunzo maalumu ya Mpango wa Uongozi wa Harvard (Harvard Ministerial Leadership Program) inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.