Featured Kitaifa

SERIKALI KUIMARISHA MFUMO WA MALIPO KWA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya   walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

Baadhi wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilaya ya Tarime mkoani Mara akizungumza mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika kupokea ruzuku wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Nyamwaga kilichopo Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa TASAF, John Chacha mara baada ya kukagua barabara katika Kijiji cha Nyamwaga iliyotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya   walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Nyamwaga kilichopo Wilaya ya Tarime mkoani Mara mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

…..

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameelekeza Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii            (TASAF) kufanya maboresho kwenye mfumo wa Kielektroni wa malipo kwa njia ya simu ya mkononi kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wanufaika wa mpango huo katika Kijiji cha Nyamwaga kilichopo Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Amesema kumekuwa na  malalamiko mengi  kutoka kwa Walengwa  kuwa mfumo huo unaotumika  sasa wa kupokea fedha kwa njia ya simu umekuwa ni kero kubwa kwa walengwa hao kutokana na changamoto katika matumizi ya mfumo huo.

Amefafanua kuwa wakati mwingine Walengwa hao wamekuwa wakilazimika kutumia vijana wao au wajukuu zao kwenda kuchukua fedha ambapo wengi wao hufikisha fedha nusu au hawafikishi kabisa.

“Tuna ushahidi wa kutosha kuwa baadhi ya vijana wanaopokea fedha kwa niaba ya walengwa hao sio waaminifu kwa kuwa wamekuwa wakizitumia fedha hizo kwa shughuli zao binafsi kusababisha walengwa hao wa TASAF kukosa hata kile kidogo ambacho Serikali imekuwa inakitoa” ameongeza Mhe.Kikwete.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha Walengwa hao wananufaika na fedha hizo, hivyo mfumo wa kupokea fedha mkononi ni njia rafiki kwa sasa kwa kundi hilo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa walengwa hao na kuhakikisha nia ya kuondoa umaskini inafika kwa wananchi wote bila kujali itikadi za kisisa.

Mhe. Kikwete yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kusikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili ili kuzitatua na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

About the author

mzalendoeditor