Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji usalama wa milki za ardhi nchini katika Halmashauri ya Chalinze uliofanyika leo Septemba 7,2023 katika ukumbi wa Kikwete.
Na.Mwandishi Wetu
Wakazi wa Chalinze wametakiwa kutoa ushirikiano kwa maafisa wanaotekeleza mradi wa Uboreshaji usalama wa milki za ardhi nchini kwa kukubali kuchangia sehemu ya vipande vyao vya ardhi kwa lengo la kutenga maeneo maalumu ya kijamii yatakayotumika kwa matumizi ya Umma kama vile shule, huduma za afya, maeneo ya michezo pamoja na barabara.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mhe. Halima Okash alipokua akifungua mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa Mradi huo katika Halmashauri ya Chalinze uliofanyika leo tarehe 07/09/2023 katika ukumbi wa Kikwete.
Aidha Mhe. Okash alisema kuwa ujio wa mradi huo utarahisisha upatikanaji wa miundombinu muhimu ya barabara ambayo imekua ni changamoto katika maeneo mengi ndani ya halmashauri hiyo jambo linalopelekea ukosefu wa huduma ya haraka pindi yanapotokea majanga ya moto, mafuriko au wagonjwa.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii wa Mradi Bi. Tumaini Setumbi amesema malengo ya kufanya mikutano ya wadau katika maeneo yatakayopitiwa na Mradio huo ni kutoa na kuboresha miongozo ya ushiriki wa wadau, kutengeneza mbinu za mawasiliano baina ya wadau na watekelezaji wa mradi ikiwemo namna sahihi ya kusambaza taarifa, kujadili namna sahihi ya kuwasilisha hoja au malalamiko yanayohusu mradi pamoja kutafakari maazimio yatokanayo na vikao ili kuboresha ufanishi wa utekelezaji wa mradi.
Chalinze ni muongoni mwa Halmshauri 41 zinakazopitiwa na mradi wa Uboreshaji usalama wa milki za ardhi, ambapo Zaidi ya viwanja 7,600 vimepimwa, huku Viwanja 50,000 vikitarajiwa kupimwa mpaka mwisho wa mradi huo.