Featured Kitaifa

DOLA MILIONI 300 KUTEKELEZA MRADI WA KILIMO KWA MFUMO WA P for R

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe
 

 

Na Nyabaganga Daudi Taraba

 

Madi wa kilimo umezinduliwa Septemba 6, 2023, kwenye ukumbi mdogo wa Ruaha uliopo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanyika katika mkutano wa AGRF 2023, Jijini Dar es Salaam.

Mradi huo umejikita katika kutekeleza masuala ya utafiti, ugani, miundombinu, na mbegu ili kuwezesha utekelezaji kufanyika.utatekelezwa kwa fedha za mkopo toka banki ya dunia ndani ya miaka mitano

Wanufaika na mradi ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na thamani ya mradi ni Dola za Kimarekani milioni mia tatu (300).

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amesema inawezekana kabisa fedha hizo zikatumika chini ya miaka mitatu hii ni kutokana na uhitaji uliopo., hivyo, amewaomba wadau husika katika masuala ya fedha kumpa ushirikiano ili mradi utekelezwe na kukamilika mapema.

Aidha, amewaomba Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa, maana wao ndio wana watu na ardhi.

Ameendelea kuasa watu kuacha kuita wakulima kuwa ni wakulima wadogo, maana huo udogo  umepimwa na kipimo gani? kipimo gani kinachotumika kuwapima ili kuwaita wadogo. Kufanya hivyo ni kuendelea kuupa umaskini nguvu.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na washirika wa maendeleo, wakiwemo Bwana Martien Van Nieuwkoot, Global Director wa Benki ya Dunia, Bw Nathan Beleth, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji wa Zanzibar, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali, na wadau wengine kutoka ndani na nje ya nchi.

Waziri alimalizia kwa kusema, kama PforR iliwezekana katika ujenzi wa madarasa, katika Kilimo pia itawezekana.

Amewashukuru wadau wote wanaoshiriki katika sekta ya kilimo, zikiwemo Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Viwanda, pamoja na Kamati ya Bajeti ya Wizara ya Fedha, na kuomba ushirikiano wao endelevu katika kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa.

 

 
 

About the author

mzalendoeditor