Featured Kitaifa

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAMPOKEA KATIBU MKUU MPYA MHANDISI CYPRIAN LUHEMEJA

Written by mzalendoeditor

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akisalimiana na Menejijimenti ya Ofisi hiyo baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo Septemba 4, 2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi hiyo leo septemba 4, 2023 katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Leonard Mchau (katikati) baada ya kuwasili katika ofisi hiyo leo septemba 4, 2023 katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobasi Katambi akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo leo Septemba 4, 2023 katika Mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akiangalia ramani ya jengo la Ofisi hiyo leo Septemba 4, 2023 katika Mji wa Serikali Mtumba, kulia ni Saudeni Anania Mkadiriaji Majenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian John Luhemeja amewasili katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma Septemba 4, 2023 na kupokelewa na Menejimenti pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Katibu Mkuu Luhemeja alikutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo.

Baada ya mapokezi hayo Mhandisi Luhemeja alikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hiyo inayojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba.

About the author

mzalendoeditor