Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dkt. Vedastus Timothy (kulia) akizungumza na wachezaji wa michezo mbalimbali wakati akizindua Bonanza la michezo lililoandaliwa na Wizara ya Fedha na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Mkuregenzi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bi. Josephine Matiro (kulia) akitoa salamu za taasisi hiyo wakati wa kufungua Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Fedha pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Kikosi cha wachezaji wa mpira wa miguu wa Timu ya Hazina wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Fedha pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Timu ya kuvuta Kamba ya Wanawake kutoka Wizara ya Fedha wakionesha umahiri wao katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Timu ya kuvuta Kamba ya Wanaume kutoka Wizara ya Fedha wakipambana na mpinzani wao katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kuruka na magunia kionesha umahiri wao katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),lililofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Na Farida Ramadhani- WF, Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zilizo chini yake wamehamasishwa kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zao na kuongeza ufanisi katika majukumu yao.
Rai hiyo imetolewa katika viwanja vya Mlimani jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dkt. Vedastus Timothy alipozindua Bonanza la michezo lililoandaliwa na Wizara ya Fedha na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Dkt. Timothy alisema lengo la kufanya bonanza hilo ni kuhamasisha watumishi kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zao na kuboresha uhusiano kati yao.
“Kazi nyingi za ofisini zinahushisha watu kukaa muda mrefu na kufanya miili kuathirika na magonjwa yasiyoambukiza kwa urahisi, kwa hiyo fursa ya kuwashirikisha watumishi kwenye michezo ni kuwawezesha kukabiliana na magonjwa hayo”, alisema Dkt. Timothy.
Naye Mkurungenzi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bi. Josephine Matiro alisema bonanza hilo linaunga juhudi za Serikali kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kuwawezesha watumishi kuwa na afya njema.
Alisema rasilimali watu ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi hivyo afya zao inabidi zilindwe ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi na kuiwezesha nchi kupata maendeleo.
Kwa upande wa Afisa Michezo wa Wizara ya Fedha, Bw. Gema Mwakyusa na Katibu wa Timu ya Michezo ya Hazina, Bw. Kelvin Kakoko, walisema bonanza hilo ni utaratibu ambao umewekwa na Wizara kila baada ya muda kuwakutanisha watumishi pamoja katika michezo ili kuhakikisha watumishi wa Wizara pamoja na taasisi zake wanakuwa na afya bora.
Akizungumza baada ya kumaliza michezo Kiongozi wa Timu ya Hazina, Bw. Asegelile Mboya, alisema pamoja na mambo mengine bonanza hilo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayotarijiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2023.
Bonanza hilo lilihusisha michozo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta Kamba, kukimbiza kuku pamoja na kuruka na magunia.