Featured Kitaifa

RAIS SAMIA  KUFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI

Written by mzalendoeditor

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam

Jeshi la Polisi Nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maafisa wakuu waandamizi kutoka Makao Makuu, Mikoa na vikosi kuanzia septemba 04, 20223 jijini Dae es salaa, kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akitoa taarifa hiyo leo septemba 02,20223 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Misime amebainisha kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalam kutoka vyuo vya hapa Nchini na wataalam wa kada mbalimbali ambapo amesema maafisa washiriki watapata fursa ya kufanya tathmini ya majukum ya Jeshi la Polisi na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa mwaka 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia SACP Misime amesema kuwa Mikutano hiyo ni utaratibu uliowekwa na Jeshi la Polisi ili kuwakutanisha maafisa wakuu waandamizi Pamoja kufanya tathmini na kuweka mikakati ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa Nchini.

Misime ameongeza kuwa Mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu isemayo matumizi ya Tehama kuleta uwazi na ufanisi katika utendaji wa Jeshi la Polisi.

About the author

mzalendoeditor