Featured

CHATANDA KUZINDUA MASHINDANO YA UVCCM SHY TOWN DR. SAMIA CUP 2023

Written by mzalendoeditor
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga na Mratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF Mkoa wa Shinyanga Magubika Amani akizungumza na waandishi wa habari
Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Mashindano maalumu ‘UVCCM Shinyanga Mjini ya Dr Samia Cup’ maarufu Samia Viwanjani yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe. Mary Chatanda kesho Jumamosi Agosti 26,2023 katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga.

Lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana wilayani humo pamoja na kuchochea maendeleo ya mchezo wa soka ambapo zawadi zitatolewa kwa bingwa, mshindi wa pili na tatu, wachezaji bora wa mechi, kipa bora, kocha, mfungaji na timu bora.
 
Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa Agosti 25,2023 Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro amesema katika uzinduzi huo vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi vitakabidhiwa.
 
“Sisi kama taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia tunaunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia kwa kuhamasisha michezo na sasa tunakwenda kufanya uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu ambayo yatashirikisha timu 32 yakifanyika kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kuanzia Agosti 27,2023 katika viwanja vinane Wilaya ya Shinyanga Mjini”,ameeleza Isaro.
 
“Mashindano haya tumeyaita Samia Viwanjani kwa kuwa tunaona Mhe. Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan anapenda michezo hivyo taasisi ya Bega kwa Bega kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini tunakwenda kufanya mashindano haya ambayo yatakuwa mashindano endelevu kwa kumuunga mkono Rais wetu kwa kupenda michezo hususani mpira wa miguu. Pia tutakuwa na michezo mingine ikiwemo Netiboli na mpira wa rede”,ameeleza.

Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari

Amesema mashindano hayo yatafanyika kwa viwango na mfano hivyo kuwaomba wananchi wa Shinyanga hususani wapenda michezo wajitokeze kwa wingi katika viwanja.
 
“Mashindano haya yataenda kwa mfumo wa mtoano kwa awamu ya kwanza, tukitoka knock out tutakuwa tumebakiza timu 16, tutakwenda tena tutabakiza timu nane, tutakwenda fainali mwisho tutatoa zawadi ikiwemo Kombe”,amesema Isaro.
 
Niwaombe vijana wote wanaoshiriki mashindano haya watambue mpira kwa sasa ni ajira, niwaombe wawe na nidhamu kwani nidhamu yao ndiyo itakayoweza kuwafikisha mbali kwani tunaenda kuibua vipaji ambavyo vitashiriki ligi mbalimbali”,ameongeza.
 
“Tunakwenda kuwaleta pamoja vijana takribani 1600. Pia tutaongea na vijana kuhusu changamoto zilizopo katika jamii. Tumeshirikisha makundi ya timu mbalimbali wakiwemo Bodaboda, timu za Masoko, Taasisi ikiwemo SHUWASA, walimu, watumishi, Veterani, kwa hiyo hatujabagua timu ya aina yoyote”,ameongeza.
 
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete ameeleza kuwa, mashindano ya Dr. Samia Cup 2023 yameanzishwa na UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama kwa lengo kuwaweka vijana pamoja lakini pia michezo ni sehemu ambayo inaajiri vijana wengi kwa kasi kubwa hivyo moja ya sehemu walizotupia jicho ni michezo hasa mpira wa miguu.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete akizungumza na waandishi wa habari
 
“Michezo hii imeandaliwa na viongozi wa CCM lakini hayanyimi fursa vijana kutoka vyama vingine, tunawakaribisha kuja kushiriki. Kupitia mashindano haya tunakwenda kuwapatia vijana fursa ili timu zinazoshiriki ngazi mbalimbali ziweze kuwaona na kuibua vipaji vyao”,amesema Madete.
 
“Wapenzi na mashabiki wa soka wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia vipaji kutoka kwa vijana wa Shinyanga pia sisi kama ofisi ya UVCCM tumepania kuhakikisha tunarudisha michezo ndani ya wilaya yetu. Boli limerudi Shinyanga”,amesema Madete.
 
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Naibu Katalambula amesema wameshirikiana na taasisi ya Bega kwa Bega na katika kuratibu na kuwezesha mashindano hayo hivyo watahakikisha mashindano hayo yanakuwa endelevu.
“Sisi kwetu CCM kufanyika kwa michezo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 lakini kama jumuiya ya vijana ni jukumu ambayo ina jukumu la moja kwa moja kwa maendeleo na kuwaweka vijana pamoja tumeamua kuratibu mashindano haya kwa nguvu na wivu mkubwa. Tunawaomba vijana washiriki katika mashindano haya kikamilifu. Tunataka tuukusanye mji wa Shinyanga pamoja, kule tutakutana na vijana mbalimbali, pia tutakuwa na soko kwani bidhaa mbalimbali za wajasiriamali zitauzwa viwanjani“,amesema Katalambula.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga na Mratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF Mkoa wa Shinyanga Magubika Amani amesema mashindano hayo ni ya wazi hakuna kiingilio huku akitaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), CCM Kambarage, Old Shinyanga Jeshini, Shule ya msingi Kitangili, Ibadakuli, Jasco Ngokolo, Shule ya msingi Ndala na Lubaga Joshoni.
 
“ Tutahakikisha sheria zote 17 za mchezo wa mpira zinafuatwa kwa hiyo taratibu zote zimefuatwa na tumetoa kibali kwa umoja wa vijana , Mashindano haya yatakuwa makubwa, naomba wadau wote wa soka wajitokeze kwa wingi. Tutahakikisha mashindano haya yanaendeshwa kwa ufanisi mkubwa ili malengo yatimie na tumechagua wataalamu mbalimbali katika viwanja vitakavyotumika kuhakikisha kwamba vijana ambao wanaonekana wapate fursa ya kuweza kuchezea timu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga na taifa”,amesema Magubika.
Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023
Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari
Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete akizungumza na waandishi wa habari
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza na waandishi wa habari
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza na waandishi wa habari
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga na Mratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF Mkoa wa Shinyanga Magubika Amani akizungumza na waandishi wa habari
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga na Mratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF Mkoa wa Shinyanga Magubika Amani akizungumza na waandishi wa habari

About the author

mzalendoeditor