Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akifafanua jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Tamasha kubwa la Kizimkazi linalotarajiwa kuanza Kesho 25 Agost,hafla iliofanyika Ofisini kwake Migombani Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Tamasha kubwa la Kizimkazi linalotarajiwa kuanza Kesho 25 Agost,hafla iliofanyika Ofisini kwake Migombani Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
Na Asya Khamis Maelezo
Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni,na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita amewataka wanajamii kuunga mkono na kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa tamasha la Kizimkazi festival ili kuchochea maendeleo na ustawi katika jamii.
Hayo yameelezwa na Waziri huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini Migombani Mjini Zanzibar.
Amesema tamasha linatarajiwa kuzinduliwa tarehe 26 mwezi huu na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe D.k Hussein Ali Mwinyi huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa shughuli mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwemo kuhamasisha watu kwenye masuala ya michezo, sanaa, na shughuli za kijamii kwa lengo la kuleta maendeleo kwa jamii husika.
Aidha amesema ushiriki wa wananchi utasaidia kujionea mafanikio ya tamasha hilo pamoja na umuhimu mkubwa katika kuchochea miradi ya maendeleo.
Waziri tabia aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliofanikisha kuunga mkono Tamasha hilo ikiwemo Zanzibar maisha bora foundation, mwanamke initiative foundation pamoja na Wizara yake inayotoa habari kwa ajili ya kuihabarisha jamii juu ya tamasha hilo
Tamasha linatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 31 mwezi huu na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika maeneo ya Kizimkazi.