Featured Michezo

YANGA SC YATUMA SALAMU LIGI KUU,YAIZAMISHA 5G KMC

Written by mzalendoeditor

MABINGWA Watetezi  Yanga SC imeanza kwa kishindo Ligi Kuu ya NBC  baada ya kuizamisha mabao 5-0 Timu ya KMC mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilienda mapumziko ikiwa inaongoza bao lililofungwa na beki bora wa Msimu uliopita Dickson Job dakika ya 17.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa KMC licha ya kufanya mabadiliko ya wachezaji mbalimbali Kiungo Mshambuliaji aliyekuwa bora katika mchezo huo Stephane Aziz Ki aliwanyanyua mashabiki wa Yanga mnamo dakika ya 59.

Akichukua nafasi ya Kennedy Musonda Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Hafiz Konkon alifunga bao la tatu dakika ya 70 huku mabao bora kwa leo yakifungwa na Viungo Mudathir Yahya dakika ya 76 na Pacome Zouzou dakika ya 81.

About the author

mzalendoeditor