Featured Kitaifa

WAWEKAHAZINA WA HALMASHAURI NCHINI WATAKIWA KUFUNGA HESABU KWA KUJIBU HOJA ZA CAG

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki,akizungumza na  Wekahazina na Wahasibu wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kikao kazi cha Ukaguzi wa Hesabu za Mwisho wa Mwaka wa Fedha Juni, 2023 kilichofanyika leo Agosti 17,2023 Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati,akizungumza na  Wekahazina na Wahasibu wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kikao kazi cha Ukaguzi wa Hesabu za Mwisho wa Mwaka wa Fedha Juni, 2023 kilichofanyika leo Agosti 17,2023 Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,Angellah Kairuki amewataka waweka hazina wa halmashauri kuhakikisha wanafunga hesabu kwa kujibu hoja za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Agosti 17,2023 jijini Dodoma amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha siku nne cha waweka hazina wa halmashauri zote nchini.

Aidha amewataka kusimamia mapato katika halmashauri kwa kuwafuatilia mienendo,historia na utaratibu uliotumika wa kuwapata mawakala wa kukusanya mapato katika halmashauri zao ili kuondokana na mianya ya upotevu.

“Wapo ambao wamepewa mashine za kukusanyia mapato lakini unakuta wengine unakuta wanazo mbili mbili, na yawezekana wengine tunawajua ni vyema tukafuatilia mienendo ya maafisa wetu wanao kusanya mapato katika vyanzo mbalimbali lakini vilevile utaratibu tunao utumia kuwapata mawakala wanao kusanya mapato katika halmashauri zetu, “amesema Kairuki.

Aidha, ameongeza kuwepo kwa usimamizi mzuri wa mawakala wanaokusanya fedha kwa kuwa wengi wao hawapeleki makusanyo sehemu husika na muda maalum.

”Tuwe macho kwa wale wanaokusanya fedha na hawapeleki makusanyo yao sehemu husika ni vyema mkafanya usimamizi mzuri”amesema Kairuki

Pia ametaka wakaangalie tena vigezo wavyotumia kuwapata mawakala hao pale wanapohitajika pamoja na kuangalia historia zao katika masuala ya kifedha.

“Pengine unaweza kukuta niwezi hawana historia nzuri halafu hatujachunguza na tunakuja kuwapa madaraka makubwa ya kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri, kwahiyo ni vyema nanyi mkaanza kufuatilia kuangalia kila chanzo,”amesema Mhe. Kairuki.

Amesema ni imani yake kuwa wataendelea kusimamia vyema vyanzo vya mapato na ukusanyaji wake na kuhakikisha wanapata mapato halisi na makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema mfumo wa kazi ambapo kwasasa wanahudumia kuanzaia ngazi ya vijiji hadi kata.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wahasibu Nchini Geogre Eston Mashauri amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuangalia hesabu zilizopita na kufanya mapitio ya ufungaji wa hesabu za mwaka huu na kutatua changamoto zote ili kuhakikisha hakuna hoja inayoweza kujitokeza.

”Katika wamefanya mapitio ya ufungaji wa hesabu kwa halmashauri zote 184,lengo likiwa ni kuangalia hesabu walizofunga mwaka jana 2021/2022 na kuangalia hesabu za mwaka wa fedha wa 2022/2023 kuishia mwezi Juni.”amesema Bw.Mashauri

About the author

mzalendoeditor