Featured Kitaifa

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUANDAA MFUMO WA RAMANI YA KIDIGITALI

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM, DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wadau imeandaa mfumo wa ramani ya kidigitali utakaowezesha wadau kupata taarifa za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Wakili Amon Mpanju akiongoza kikao kazi cha kupitia utendaji kazi wa mfumo huo jijini Dodoma Agosti 17 2023, amebainisha kuwa, lengo ni kutatua changamoto zote za awali zilizokuwa zinaonekana katika kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, hasa katika kufahamu miradi inayotekelezwa na Mashirika hayo na kwa namna gani imesaidia kutatua changamoto za Jamii na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

Mpanju ameongeza kwamba, Mfumo huo umeandaliwa kwa lengo la kurahisisha utendaji kwa wadau wote ikiwemo Serikali, Wafadhili, Mashirika yenyewe na wananchi kwa ujumla kwani utapunguza urasimu na kuleta uwazi kwa pande zote hivyo kuchochea Mashirika hayo kutimiza majukumu yao ipasavyo.

About the author

mzalendoeditor