Featured Kitaifa

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA TAMASHA LA ACCES, WADAU WA MUZIKI ZAIDI YA 1000 DUNIANI KUSHIRIKI

Written by mzalendoeditor

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya kikao na Mkurugenzi wa Taasisi ya “Music in Africa Foundation na ACCES Eddie Hatitye Agosti 14, 2023 jijini Dodoma kuhusu tamasha la ACCES ambalo litafanyika hapa nchini Novemba 9-11, 2023. 

Viongozi hao wamejadiliana namna bora ya kuendesha tamasha hilo kwa kuwashirikisha wasanii wote nchini wakiwemo chipukizi na walifanikiwa katika uga wa muziki.

Lengo la tamasha hilo ambalo linandaliwa na Taasisi ya Music in Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania ni kuwasaidia wanamuziki kutambuana na kuonyesha uwezo wao wa kuimba pamoja nakufundishwa namna ya kuchangamkia fursa za masoko.

Tamasha hilo la ACCES linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wa muziki zaidi ya 1000 kutoka zaidi ya mataifa 50 duniani ambalo kwa Tanzania linafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka jana lilifanyika Novemba 24-26, 2022 jijini Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor