Featured Kitaifa

EWURA YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI WANGIN’GOMBE

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Claudia Kitta, akitoa hotuba ya ufunguzi, wa taftishi hiyo, leo Agosti 10, Tar.10/08/2023

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Maji na Usafi wa Mazingira, Mha. Vaileth Iramu, akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya Wananchi walio hudhuria mkutano huo wakitoa maoni yao juu ya Ombi la Kurekebisha bei za maji katika mkutano huo

Na.Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekusanya maoni ya wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe juu ya ombi la kurekebisha bei za huduma za majisafi na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Wanging’ombe (WSSA).

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Claudia Kitta, aliwaasa wananchi kutoa maoni yao kizalendo, ili wapate bei zinazoendana na huduma bora za maji.

Kaimu Mkurugenzi wa Wanging’ombe WSSA, Bw. Michael Mwenda, alisema marekebisho ya bei yatasaidia mamlaka kumudu gharama za uendeshaji, kuongeza muda wa upatikanaji wa huduma, kutibu maji, upanuzi wa mtandao wa maji, kupunguza upotevu wa maji, kupunguza gharama za maunganisho mapya, kukidhi gharama za umeme na kutatua changamoto mbalimbali za huduma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Violeth Iramu, alisema, mkutano huo ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na EWURA, kupata maoni ya wadau kabla ya kutoa uamuzi kuhusu bei za maji.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao, wameiomba Wanging’ombe WSSA, kutunza vyanzo vya maji pamoja na kuongeza ufanisi katika kukusanya mapato ili kutatua changamoto zinazowakabili.

About the author

mzalendoeditor