Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na Balozi wa Japan nchini Tanzania Balozi Yasushi Misawa kujadiliana kuhusu ushirikiano katika sekta ya elimu ikiwemo uendelezaji mafunzo Vyuo vya Ufundi ambapo kwa sasa inapewa msukumo mkubwa ili kuwawezesha vijana kupata Ujuzi.
Majadiliano hayo yamefanyika leo Agosti 7, 2023 Mkoani Mbeya, ambapo pia wamezungumzia umuhimu wa kuongeza fursa za ufadhili wa masomo kwa Watanzania katika Elimu ya Juu nchini Japan.
Balozi Yasushi ameeleza kwamba takribani Watanzania 40 kila mwaka wanapata nafasi ya kwenda kusoma nchini Japan kupitia Skolashipu ya African Business Education (ABE).
Ameongeza kuwa kupitia Skolashipu ya Wizara ya Japan ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (MEXT) kila mwaka Watanzania watano hupata nafasi ya kwenda Japan kusoma kada mbalimbali ikiwemo Uhandisi na Teknolojia.