Featured Kitaifa

WANUFAIKA WA BBT – LIFE WAMKOSHA KATIBU MKUU KIONGOZI

Written by mzalendoeditor

 

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza kulia) akikagua mifugo inayonenepeshwa katika Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” (BBT – Life) baada ya kufika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambapo amesema ameridhishwa na jitihada zinazofanywa na wanufaika wa programu hiyo na kuwataka kuongeza juhudi zaidi.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza kulia) akipata maelezo ya vyakula vya mifugo vinavyotumika kwa ajili ya kunenepeshea mifugo kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” (BBT – Life) Bi. Rest Mgonja, baada ya kufika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi,

Mmoja wa wakufunzi wa wanufaika wa Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” (BBT – Life) Sekta ya Uvuvi Bw. Hamisi Salehe akimuelezea Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka namna wanavyotoa mafunzo kwa wanufaika jinsi ya kunenepesha viumbe maji wakiwemo kaa na jongoo bahari. Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Kusiluka amefika kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, akiwa na baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Mifugo wakati akikagua muonekano wa kizimba kwa ajili ya kufugia samaki wakati alipofika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Na. Edward Kondela

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka amewaasa vijana waliopo kwenye Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” (BBT – Life) kufanya vizuri zaidi kwa kutumia fursa waliyopata ili kufikia malengo ya serikali.

Mhe. Balozi Kusiluka amebainisha hayo leo (07.08.2023) katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane), kushuHUdia kwa vitendo maendeleo ya programu hiyo.

Amewataka vijana hao ambao wapo kwenye programu ya BBT – LIFE kwa vitendo katika unenepeshaji wa ng’ombe, kaa na jongoo bahari pamoja na ulimaji wa zao la mwani, kufikia maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameasisi programu hiyo ili kuwezesha vijana kiuchumi.

Ameongeza kuwa ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na vijana hao na kuwataka kuongeza jitihada zaidi kufikia maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo ni vyema wakatumia vizuri fursa waliyoipata.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema wizara imeweka mpango maalum kwa vijana hao baada ya kumaliza mafunzo kwa kuwapatia maeneo kwa mkataba wa miaka mitano pamoja na mtaji watakaokuwa wamepata wakati wa mafunzo ili kuendeleza biashara ya kunenepesha ng’ombe.

Naye mmoja wa wanufaika wa programu ya BBT – LIFE Sekta ya Mifugo, Bi. Rest Mgonja amesema wameshiriki kwa kupewa maeneo na mitaji pamoja na kununua ng’ombe ambapo kila kijana alipatiwa ng’ombe kumi na kuwa na jumla ya ng’ombe 2,400 kwa vijana 240 kwa ajili ya kunenepesha na kuwauza baada ya miezi mitatu, ambapo tayari wameuza ng’ombe 565.

Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa wanufaika wa BBT – LIFE Sekta ya Uvuvi Bw. Hamisi Salehe amemuelezea Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Kusiluka namna wanavyotoa mafunzo kwa wanufaika jinsi ya kunenepesha viumbe maji wakiwemo kaa na jongoo bahari kwa kuyaongezea thamani mazao hayo na kuuzwa kwa thamani ya juu zaidi.

About the author

mzalendoeditor