Featured Kitaifa

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUTOA FURSA KWA WATUMISHI WANAOWAONGOZA ILI WAONESHE UWEZO WAO KIUTENDAJI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa  ziara yake ya kikazi  katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam  ikiwa ni mwendelezo wa kuzungumza na Watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza   kuzungumza na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) jijini Dar es Salaam kabla ya kuzungumza nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali   mara baada ya kuzungumza na Watumishi hao jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Ernest Mabonesho  akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kuzungumza na Menejimenti ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali, Cpt. William Budodi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kuzungumza na watumishi wa Wakala hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi mara baada ya Waziri huyo kuzungumza na watumishi wa Wakala hiyo jijini Dar es Salaam.

Na. Lusungu Helela-Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watendaji Serikalini kuwapa nafasi watumishi walio chini yao ili waweze kuonesha uwezo wao kiutendaji kwa lengo la kuchagiza dhana ya utawala bora badala ya kuhodhi kila kitu.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo  wakati wa ziara yake ya kikazi  katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

‘’Ukiwa Kiongozi, hakikisha unaacha alama katika eneo unaloliongoza kwa kuwaandaa watumishi kiutendaji ili unapostaafu au kuondoka eneo hilo kwa taratibu nyingine, basi halitatetereka huku heshima yako ikibaki kama Kiongozi wa mfano katika mioyo ya watu’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene amesema anatamani kuona Taasisi zote za Serikali zinakuwa na mtazamo huo wa kutoa nafasi kwa Watumishi wao huku akisisitiza kuwa watumishi wenye uwezo wasifichwe kwa hofu ya wenye mamlaka kupokwa nafasi zao kwani serikali bado ina kazi nyingi sana.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene ameonya tabia ya baadhi ya Watendaji katika Taasisi za Serikali kukaimisha nafasi za uongozi kwa watumishi wasio na sifa wakati wanaostahili kupewa nafasi hizo wapo.

Akizungumza na watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali, Mhe. Simbachawene amesema watumishi wanaokaimishwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wanapaswa kuwa na sifa za kushika nafasi hizo ili kuirahisishia Ofisi ya Rais – UTUMISHI mchakato wa kuwathibitisha.

“Naomba niwaambie ukweli, ukimkaimisha Mtumishi ambaye hana sifa, inatuwia vigumu kumthibitisha kwani anakuwa hana vigezo kwenye nafasi hiyo” amesisitiza Mhe. Simbachawene. 

Aidha, Waziri Simbachawene ameelekeza kufanyiwa kazi kwa changamoto mbalimbali zinazokwamisha utendaji kazi wa watumishi katika maeneo yao ya kazi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wao, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka wakiongea kwa nyakati tofauti wamemshukuru Waziri Simbachawene kwa kuweka utaratibu wa kuwatembelea watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuelekeza zifanyiwe kazi kwa maslahi mapana ya taifa.

Viongozi hao wameahidi kuzifanyia kazi changamoto za watumishi ambapo wamesema tayari nyingine zimeshaanza kufanyiwa kazi.

About the author

mzalendoeditor