Klabu ya Yanga imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji, Hafiz Konkoni (23) Bechem United ya Ghana kwa kandarasi ya miaka miwili.
Konkoni ambaye amesajiliwa kuziba pengo la Mkongomani Fiston Mayele anayetajwa kujiunga na Pyramid ya Misri baada ya msimu uliopita kumaliza na mafanikio ya kuwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Mrsimu uliopita katika ligi ya Ghana alifanikiwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 26 na kutoa assist 3 akimaliza nafasi ya pili.
Kabla ya Konkoni kusajiliwa na Yanga alikuwa akihusishwa klabu ya Al Hilal ya Sudan.