Featured Kitaifa

TBS YASHINDA TUZO TAASISI BORA YA UDHIBITI AFRIKA.

Written by mzalendoeditor
Na Grace Semfuko, MAELEZO.
 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeshinda Tuzo ya kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti kwa Mwaka 2023 zilizoandaliwa na Taasisi ya African Leadership Magazine ambayo ilishirikisha makundi mbalimbali kutoka nchi Tofauti Barani Afrika.
 
TBS iliteuliwa kuwa kati ya taasisi mbili za Afrika zilizoingia katika kinyang’anyiro hicho katika mzunguko wa 13 wa tuzo hizo huku taasisi nyingine ikiwa ni Food and Drugs ya nchini Ghana.
 
Akiwasilisha tuzo hiyo kwa watanzania leo Julai 28, 2023, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Wizara yake inasimamia na kuhakikisha inawajengea mazingira bora na wezeshi kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Sekta ya Viwanda ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora za kushindaniwa katika soko la Dunia.
 
“Nami kama Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo TBS ni sehemu, ninajivunia mafanikio haya makubwa kwani yanatuweka katika ramani ya Bara la Afrika, lakini pia ni chagizo katika masuala ya viwango kwani ni kielelezo tosha kuwa Tanzania ni nchi yenye mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara, nina imani pia kwamba tuzo hii itakuwa kivutio kwa bidhaa zetu kupata soko ndani na nje ya nchi. Tuzo hii imekuwa ni motisha na chachu kwetu na tunaahidi kuendelea kuwatumikia wananchi na kuwahakikishia mazingira ya ubora wa bidhaa sokoni na kulinda afya ya mlaji” amesema Dkt. Kijaji.
 
Amesema tuzo hiyo ni ishara ya kwamba agenda ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kuwepo kwa mazingira wezeshi ya biashara nchini imefanikiwa ndani ya TBS mafanikio ambayo yanaitangaza Tanzania katika sekta ya Viwanda na Biashara, pia ni kielelezo cha umahiri, ufanisi na weledi katika masuala ya viwango ikiwa ni Pamoja na udhibiti ubora na usalama Barani Afrika.
 
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Profesa Othman Chande amesema Mei 08 Mwaka huu Shirika hilo liliteuliwa kuwa kati ya taasisi mbili Barani Afrika zilizoingia katika kinyang’anyiro cha kushindania tuzo ya kuwa taasisi bora ya udhibiti ya mwaka 2023.
 
“Tuzo hizi za African Busines Leadership Awards ambazo huandaliwa na Taasisi ya African Leadership Magazine hushirikisha makundi mbalimbali kutoka nchi tofauti Barani Afrika ambapo TBS ilitangazwa mshindi, Pamoja na Ushindi wa TBS Tanzania iliwakilishwa vema na Mkurugenzi wa Mohammed Enterprises Bw. Mohammed Dewji aliyeshinda tuzo ya African Busines Leader of the Year 2023, Ally Edha Awadh Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Oil aliyeshinda Young African Energy Leader of the Year 2023 na Tanzania Portland Cement PLC iliibuka mshindi wa pili kama African Company of the Year 2023” amesema Prof. Chande.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akipokea Tuzo ya TBS kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti kwa Mwaka 2023 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande na kuiwasilisha tuzo hiyo kwa Watanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo ya TBS kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti kwa Mwaka 2023 na kuiwasilisha tuzo hiyo kwa watanzania. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande akizungumza katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiwa kwenye hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiwasilisha tuzo kwa watanzania, tuzo ambayo TBS imeshinda kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti kwa Mwaka 2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akipata picha ya pamoja na Watumishi wa TBS katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande wakati akiwasili Makao Makuu ya TBS katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya wakati akiwasili Makao Makuu ya TBS katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Simpeho Nyari wakati akiwasili Makao Makuu ya TBS katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Simpeho Nyari wakati akiwasili Makao Makuu ya TBS katika hafla ya kuwasilisha Tuzo ya TBS Kuwa Taasisi Bora ya Udhibiti Afrika kwa Mwaka 2023, hafla ambayo imefanyika leo Julai 28,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
 
 
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

About the author

mzalendoeditor