Featured Kitaifa

WAZIRI KIJAJI ATAKA WAZALISHAJI BIDHAA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA KUKABILIANA NA KUPANDA KWA BEI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Viwanda na biashara Dk.Ashatu Kijaji  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 25,2023 jijini Dodoma  kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa Kwa mwaka 2022/2023 kwa kipindi kilichoanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 

Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAZIRI wa Viwanda na biashara Dk.Ashatu Kijaji amewataka wazalishaji wa bidhaa zote za viwandani kuongeza jitihada za uzalishaji wa bidhaa kwa ubora unaohitajika sokoni na kwa kufuata
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa nchini.

Dk.Kijaji amezungumza hayo leo Julai 25,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa Kwa mwaka 2022/2023 kwa kipindi kilichoanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 na kusisitiza kuwa hatovumilia kuona mzalishaji, msambazaji au muuzaji wa bidhaa yoyote ile akiongeza kiholela bei ya bidhaa yoyote ile bila sababu ya msingi.

Kutokana na hayo amewaelekeza maafisa biashara wote nchini waliopo kwenye Halmashauri zao kuhakikisha wanasimamia suala hilo la bei za bidhaa ipasavyo na kwamba wao ndiyo wenye jukumu la kuwalinda wazalishaji na walaji pia.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ameeleza kuwa uzalishaji wa mazao muhimu ya chakula nchini kwa mwaka 2021/2022 ulikuwa ni takribani tani milioni 17.15 ikiwa ni pungufu kwa tanimilioni 1.52
ukilinganisha na uzalishaji wa mazao hayo kwa mwaka 2020/21.

Amesema,”Mazao muhimu yanayotajwa hapa ni pamoja na mahindi, mchele, ngano, mtama,
uwele, ulezi, mihogo, maharage na mikunde, ndizi na viazi,kupungua huko kwa uzalishaji kulisababishwa na mtawanyiko wa unyeshaji wa mvua usioridhisha,”amefafanua

Katika taarifa hiyo ya mwaka ya mwenendo wa bei za mazao na bidhaa za vyakula,Dk.Kijaji amesema wanangalia mazao ya mahindi, mchele, maharage, ngano na viazi mviringo ikiwa ni pamoja na bidhaa nyingine za vyakula ikiwemo unga wa mahindi, unga wa ngano pamoja na mafuta ya kupikia.

Afafanua kuwa,”uzalishaji wa mahindi kwa mwaka 2021/2022 ulikuwa ni tani milioni 6.417
ambazo zilikuwa pungufu kwa tani 620,000 ukilinganisha na uzalishaji wa mwaka 2020/2021uliokuwa tani milioni 7.039. Sehemu ya kiasi hicho cha mahindi kilichozalishwa katika mwaka 2021/2022 ndicho kilichoingia katika msimu wa masoko ya mazao wa mwaka 2022/2023,”amesema na kuongeza;

Hivyo, ni dhahiri kuwa ugavi wa mahindi kwa mwaka 2022/2023 uliathirika kutokana na kupungua
kwa uzalishaji na hivyo kusababisha bei ya mahindi kwa walaji kuwa ya juu,katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 wastani wa bei ya chini ya mahindi ilikuwa ni Shilingi 771 kwa kilo, wakati wastani wa bei ya juu ilikuwa ni Shilingi 1,612 kwa kilo,”amesema

Dk.Kijaji pia ameeleza kuwa Miezi iliyokuwa na bei ya chini kuliko yote katika kipindi hicho ni Julai, Agosti, Octoba na Novemba2022 pamoja na mwezi Juni 2023 kwa bei ya Shilingi 700 kwa kilo na kwamba, mwezi Desemba 2022 ulikuwa na bei ya juu kuliko miezi yote katika kipindi husika kwa bei ya
Shilingi 1,890 kwa kilo.

“Hata hivyo, uchambuzi wa bei ya wastani ya mahindi nchini bila kujali bei ya chini au bei ya juu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilikuwa ni Shilingi 1,200 kwa kilo,”amesema

Kwa upande wa bidhaa za Ujenzi, ameeleza kuwa hadi kufikia Juni, 2023, Tanzania ina viwanda vya saruji vipatavyo 14 ambapo kati ya hivyo,viwanda7 ni vikubwa (intergrated plant)na vilivyobakia
vinazalisha saruji kutokana na clinker iliyozalishwa na viwanda hivyo saba.

Ameeleza kuwa takwimu za uzalishaji wa saruji kwa mwaka 2022, zinaonesha kuwa viwanda vya saruji nchini vinazalisha tani 10,850,000 za saruji kwa mwaka ambapo mahitaji ya ndani ya nchi ni tani 7,100,000 kwa mwaka.

Amefafanua kuwa , kuna ziada ya tani 3,750,000 ambayo huuzwa katika soko la nje hususan katika nchi za Congo, Rwanda, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 uchambuzi uanonesha kuwa kwa wastani, saruji aina ya 32.5R iliuzwa kwa ya Shilingi 17,009 kwa mfuko wa kilo 50,Wastani wa bei ya chini ya saruji ya aina hiyonchini kwa kipindi hicho ilikuwa ni Shilingi 14,203 huku mwezi Julai 2022 ukiwa na bei ya
chini kuliko miezi yote kwa Shilingi 12,500 kwa mfuko wa kilo 50,”amefafanua

Pia,wastani wa bei ya juu ya saruji ya aina hiyo ilikuwa ni Shilingi 22,923 kwa mfuko wa
6bei yake imepanda kwa asilimia 1.4 ukilinganisha na wastani wa bei ya bidhaa hiyo kwa mwezi Juni 2023.

“Bei ya Nondo mm 10 kwa mwezi Julai 2023 ni kati ya Shilingi 11,750 na 18,000,Bei hiyo imeonesha uhimilivu kwa kutokuwa na mabadiliko yoyote ya bei ya juu au bei ya chini ukilinganisha za bei ya mwezi Julai 2023 na mwezi Juni 2023,bei za chini zipo katika mkoa wa Tabora na bei ya juu ipo katika
mkoa wa Iringa huku bei ya nondo mm 12 kwa mwezi Julai 2023 ni kati ya Shilingi 22,000 na
28,000;

Bei hiyo imeonesha uhimilivu kwa kutokuwa na mabadiliko yoyote ya bei ya juu au bei ya chini ukilinganisha bei za mwezi Julai 2023 na mwezi Juni 2023. Bei za chini zipo katika mkoa wa Dar es Salaam na bei ya juu ipo katika mikoa ya Rukwa na Katavi,”amesema.

Kwa upande wa bati ameeleza kuwa bei ya bati nyeupe geji 30 kwa mwezi Julai 2023 ni kati ya Shilingi 21,500 na 27,000 na Kwamba bei hiyo imeonesha uhimilivu kwa kutokuwa na mabadiliko yoyote ya
bei ya juu au bei ya chini ukilinganisha za bei ya mwezi Julai 2023 na mwezi Juni 2023.

About the author

mzalendoeditor