Featured Kitaifa

SPIKA DKT.TULIA ATETA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CAMEROON

Written by mzalendoeditor

Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cameroon, Mhe. Felix Mbayu katika Ofisi za Waziri huyo zilizopo Jijini Yaounde nchini Cameroon leo tarehe 21 Julai, 2023.

Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cameroon, Mhe. Felix Mbayu katika Ofisi za Waziri huyo zilizopo Jijini Yaounde nchini Cameroon leo tarehe 21 Julai, 2023.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemshukuru Waziri huyo kwa niaba ya Mawaziri wengine ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Mawaziri ya Umoja wa Afrika (AU) kwa kupitisha jina lake kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) anayeungwa mkono na AU.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

About the author

mzalendoeditor