Featured Kitaifa

BUWSSA YAWEKA MIKAKATI MBALIMBALI KUONGEZA UPATIKANAJI WA MAJI

Written by mzalendoeditor

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Bi.Ester Gilyoma ,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20,2023 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaya hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA),imeweka mikakati mbalimbali ya kuongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 77 iliyopo sasa hadi kufikia zaidi ya asilimia 95 ifikapo mwaka 2025 kupitia miradi ya kimkakati iliyojipanga kuitekeleza na kuikamilisha.

Hayo yamesemwa leo Julai 20,2023 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Bi.Ester Gilyoma wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Amesema ametaja mikakati hiyo ni kupunguza upotevu wa maji wa miaka mitatu ulioanza mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024 unaoendana na mpango wa kibiashara wa Mamlaka ya maji

”Mwaka wa fedha wa 2022/2023 ,upotevu wa maji ni asilimia 36 ambapo katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, imeweka mikakati mbalimbali ya kupunguza upotevu huo ikiwemo kuondoa mita goigoi za maji 6,000 kwa awamu ya kwanza.”amesema Bi.Ester

Amesema kuwa Mkakati mwingine ni pamoja na mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji unaogharimu Shilingi Milioni 756.

Hata hivyo Bi.Ester amesema kuwa BUWSSA  imeandaa andiko mradi kwa ajili ya kukopa fedha kiasi cha TShs 815,000,0000 mfuko wa maji ili kuhakikisha upotevu wa maji unapungua kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024.

“BUWSSA  ina uwezo wa kuzalisha maji kutoka kwenye chanzo kipya na cha zamani Nyabehu lita za ujazo 15,264,000 /siku ambayo hayajatibiwa na lita za ujazo 10,320,000/kwa siku ambayo yametibiwa kutoka kwenye chanzo ambacho kimekamilika mwaka 2023,”alisema.

Kuhusu hali ya huduma ya maji ma Usafi wa mazingira alisema kuwa Kwa sasa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda haina huduma ya majitaka,hivyo magari ya watu binafsi ambayo yanasimamiwa na Halmashauri ya mji wa Bunda ndiyo yanatumika katika kutoa huduma za majitaka.

“Hivyo kupitia Mamlaka ya maji Bunda kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tunategemea kuanza kujenga miundo mbinu ya majitaka eneo la Butakale liliyoko Mjini Bunda,

Aidha Idadi ya wateja Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda ina jumla ya wateja 7,556 kati ya hao kuna wateja wa Nyumbani,Taasisi na Biashara,”alieleza.

BUWSSA hutoa majisafi kwa wakazi wa Bunda mjini na viunga vyake, hii inajumuisha mitaa ya Nyabehu, Guta, Tairo, Nyantare na Migungani ambayo bomba kuu linaloleta maji Bunda mjini limepita.

”Kwa kuzingatia sensa ya watu na makazi ya 2022; Wakazi wanaoishi kwenye eneo ambalo Mamlaka inatoa huduma ya maji ni watu 182,970 (2022),Kwa sasa inakadiriwa kuwa eneo linalo hudumiwa na Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda una wakazi 191,570 kati ya hao asilimia 76.7 % ndiyo wanaopata huduma kwa sasa ambayo ni sawa na wakazi 146,934 kufikia mwezi Juni 2023.”amesema

Aidha ametoa rai kwa wananchi wa Bunda kuendelea kutunza miradi hiyo ambayo serikali imewekeza kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadae na kuacha wizi wa maji.

About the author

mzalendoeditor