Featured Kitaifa

TARURA YAAHIDI KUTUNZA MAGARI YALIYOTOLEWA NA SERIKALI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki,akikata utepe kuashiria ugawaji wa Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA),Mhandisi Victor Seff ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Lazaro Londo ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki,akikata utepe kuashiria ugawaji wa Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

Muonekano wa Magari 43 yaliyotolewa kwa ajili ya Makatibu Tawala wa Mikoa 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kukabidhi Magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) kwa Makatibu Tawala wa Mikoa leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI) Angelah Kairuki ameutaka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuyatunza na kuyasimamia ipasavyo magari yaliyotolewa na Serikali  ili ili yaweze kukidhi matarajio na malengo waliyojiwekea.

Pia ameagiza magari hayo  kuhusika katika   suala la usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara za vijijini na mijini ili kuchochea shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo yao.

Akizungumza leo Julai 5,2023,jijini Dodoma katika hafla ya kukabidhi magari 43 kwa TARURA na Makatibu Tawala wasaidizi sehemu ya miundombinu,Waziri Kairuki amesema  TARURA inatakiwa  , kuyatunza na kuyasimamia ipasavyo magari hayo.

“Wasimamie  kwa mujibu wa miongozo na taratibu zilizopo ili yaweze kukidhi matarajio na malengo tuliojiwekea, kubwa likiwemo suala la usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi na ukarabati wa Miundombinu ya Barabara za Vijijini na Mijini ili kuchochea shughuli za maendeleo ya Wananchi katika maeneo yao,”amesema Waziri Kairuki.

Amesema  Serikali ya awamu ya sita  itaendelea  kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora kwa wananchi na Tarura  kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari ili kuimarisha utendaji kazi na usimamizi wa miradi.

Amesema hadi sasa Wakala imefanya manunuzi ya magari 270, ambapo Magari hayo yamekuwa yakiwasili kwa vipindi tofauti, na kukabidhiwa kwa wahusika.

“Aidha, tukumbuke kuwa hivi karibuni TARURA ilikabidhiwa Magari mengine 54 na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango. 

Hivyo, katika kuendelea kupokea Magari hayo, leo nitakabidhi Magari mengine 43, na hivyo kufanya Magari yaliyokabidhiwa kuwa 241, tangu Wakala ulipoanza ununuzi wa Magari Julai 2017 hadi Juni 2023,”amesema Kairuki

Amesema lengo la ununuzi wa magari haya ni kuendelea kuimarisha usimamizi wa shughuli za Serikali katika Sekta ya miundombinu kwa kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Waziri Kairuki amesema magari haya yatasaidia kurahisisha huduma ya usafiri kwa watendaji wa TARURA   na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu ya Miundombinu katika kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli ujenzi katika Mikoa.

Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa utendaji kazi unaimarishwa kwa kuwa na vyombo vya usafiri vya uhakika, vitendea kazi, Ofisi na watumishi makini wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

“Kutokana na majukumu yaliyopo, Magari haya yatagawiwa kwenye Ofisi za TARURA na Ofisi za Sekretatieti za Mikoa zenye changamoto na uhitaji zaidi wa Magari kwa sasa, na zenye maeneo makubwa ya kusimamia.

Amesema Sekretarieti za Mikoa zitakazapata magari awamu hii ni Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Mara, Lindi, Dodoma, Tabora na Tanga.

 Kwa upande wake Mtendaji Mkuu Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA),Mhandisi Victor Seff amesema ununuzi wa magari hayo ni mwendelezo wa Serikali ya awamu ya sita katika  kuondoa changamoto ya vitendea kazi hasa katika eneo la ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo  ya barabara kupitia ofisi za Wakuu wa Mikoa na Tamisemi.

Amesema jumla ya magari 26 yameagizwa kwa ajili ya ufuatiliaji utakaofanywa na makatibu Tawala wasaidizi sehemu ya miundombinu ambapo kati ya hayo magari 13 yameishapokelewa na 13 bado hayajapokelewa.

Amesema kwa upande wa TARURA  tangu iliponzishwa mwaka 2017  jumla ya magari 270 yamenunuliwa ikiwa ni pomoja na magari  43 ambapo magari 29 kati ya 270 bado hajapokewa.

Mhandisi Seff  amesema TARURA mpaka sasa itakuwa na magari  483 kati ya 592 yanayohitajika katika ngazi za  makao makuu,mikoa na wilayani.

Amesema tathimini waliyofanya wamebaini kati ya magari 483 waliyonayo magari mazima ni 362 yenye hali nzuri na mabovu   magari  121 hivyo bado kuna upungufu wa magari  230 sawa na asilimia 43.

Amesema  mikakati waliyoanyo ni  kuendelea kununua magari kupitia bajeti za kila mwaka  ambapo kwa mwaka 2023-2024 jumla ya  Sh bilioni 4 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa magari 40.

Akitoa utekelezaji wa kazi za ujenzi na matengenezo ya  barabara za wilaya katika mwaka wa fedha   2022-23  amesema  utekelezaji wa kazi kwa ujumla umefikia asilimia 85 ambapo  jumla ya Sh bilioni 621 zimetumika kati ya Sh bilioni  653 zilizopokelewa  sawa na asilimia 94.

Amesema fedha zilizopokelewa ni asilimia 85 ya bajeti ya  mwaka 2022-2023 ambayo ni Sh bilioni 676 kwa fedha za ndani.

About the author

mzalendoeditor