Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.

2.Amemteua Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Balozi Mapuri ameteuliwa kuwa Mjumbe kwa kipindi cha pili.

3.Amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza tarehe 01 Julai, 2023.

4.Amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA). Prof. Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili.

5.Amemteua Bw. Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 

Uteuzi huu umeanza tarehe 25 Juni, 2023.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor