Featured Kitaifa

SIMBACHAWENE ATOA MAAGIZO TAASISI ZA UMMA KUWA NA MIKATABA HAI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene,akizindua mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu  Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Juma Mkom,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter Mtwale,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene,akizindua mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania(TBA),Daud Kondoro,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya taasisi za umma mara baada ya Waziri wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene,kuzindua  mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene ameagiza taasisi zote za umma ziwe na mikataba ya huduma kwa wateja iliyo hai pamoja na kujenga uelewa kwa wateja kuhusu mikataba hiyo.

Akizungumza leo Juni 23,2023,jijini Dodoma katika uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma,Waziri Simbachawene amesema matumizi ya mikataba hiyo yameleta mafanikio kadhaa ikiwemo kuwezesha watumishi kuongeza uwajibikaji na nidhamu kazini.

Pia amesema  imeongeza watumishi  wa umma kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati.

Waziri Simbachawene amesema pamoja na mafaniko hayo yapo mapungufu ambayo yamejitokeza ikiwemo kukosekana na kutohuishwa kwa mikataba  ya huduma kwa wateja.uelewa mdogo wa  kuhusu mikataba hiyo na usimamizi usioridhisha .

Kutokana na changamoto hizo Waziri Simbachawene ameagiza taasisi zote za umma ziwe na mikataba ya huduma kwa wateja iliyo hai pamoja na kujenga uelewa kwa wateja kuhusu mikataba hiyo.

“Nina Imani  kuimarika kwa matumizi  ya mifumo ya utendaji kazi serikalini  hususani matumizi ya mikataba  ya huduma kwa wateja italeta mageuzi makubwa ya utendaji  unaojali matokeo.

“Pia kutakuwa na ungezeko  la uwajibikaji ufanisi katika matumizi  ya rasilimali nyingine katika sekta za umma.Napenda kuchukua nafasi ya  kuzipongeza taasisi za umma ambazo zimetekeleza  maelekezo husika,”amesema Waziri Simbachawene.

Amesema serikali ina jukumu la kuwezesha wananchi kupata huduma bora  ikiwa ni pamoja na elimu,afya,maji ,mawasiliano  ambapo ili kufanikisha jambo hilo Serikali ina sanifu na kujenga mifumo.

Kwa upande,Katibu Mkuu  Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Juma Mkomi amesema taasisi za umma zimekuwa zikiadhimisha wiki ya utumishi wa umma ambayo hufanyika kila mwaka. kuanzia Juni 16 hadi 23 kwa lengo la kutambua mchnago wa watumishi wa umma katika maendeleo ya nchi zao.

Amesema katika kuadhimisha wiki hiyo,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma inazindua mikataba  mikataba ya huduma kwa mteja na taasisi za umma.

Bw.Mkomi amesema mkataba huo ni ahadi ya kimaandishi kati ya taasisi ya umma na wateja wake ambapo mkataba huo unamwezesha mteja kufahamu huduma  zinazotolewa  na taasisi za uuma,viwango vya utoaji huduma,wajibu wa taasisi.

“Ni azma ya Serikali kuhakikisha kila taasisi inakuwa na mkataba wa huduma kwa wateja na kuutekeleza ipasavyo  ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma,”amesema Katibu Mkuu huyo.

Amesema katika kufanikisha hilo hilo,ofisi yake ilitoa maelekezo kwa taasisi zote za umma kuhuisha mikataba ya huduma kwa wateja na kuhakikisha taasisi zote zinakuwa na mikataba hai.

Naye  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter Mtwale ,amesema kuwa mikoa yote nchini pamoja na serikali za mitaa nchini  kuandaa mikataba na kusimamia mikataba kwa watumishi wa umma katika kutekeleza utekelezaji  ambao umeandikwa kisheria lakini tujali majukumu ambayo tunatakiwa kuyafanya,

” Nikiiri kwamba bado mikataba ya watumishi wa umma katika ofisi za serikali ya mitaa bado hatuja zingatia katika ngazi ya mikoa na mitaa hivyo tunaenda kutekeleza hilo” amesema Mtwale 

About the author

mzalendoeditor