Uncategorized

VIFAA VITAKAVYOTUMIKA KATIKA MBIO ZA JKT MARATHON 2023 VYAZINDULIWA RASMI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Elimu,Utamaduni na Michezo JKT  Kanali Erasmus Bwigoge ,akionyesha jezi pamoja na Vifaa vya Michezo vitakavyotumika katika Mbio za JKT Marathon 2023 jijini Dodoma.

Na. Gideon Gregory-CHAMWINO 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limezindua vifaa vya michezo vitakavyotumika katika mbio za JKT 2023 zinazotarajiwa kufanyika Juni 25 mwaka huu katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais mstaafu  wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete.

Akizindua vifaa hivyo leo Juni 16,2023  Mkurugenzi wa Elimu,Utamaduni na Michezo JKT  Kanali Erasmus Bwigoge amesema mbio hizo ni miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanyika kuelekea kilele Cha maadhimisho ya miaka 60 ya JKT tangu kuanziashwa kwake.
Amesema viifaa vilivyozinduliwa ni pamoja na T-shirt ,medali,alama za mkononi na namba ambavyo vyote vitatumika katika mbio hizo.
Aidha amesema katika mbio hizo kutakuwa na mbio za kilometa Tano,10 na 21.1 huku akisema Kila mbio itakuwa na barabara zake za kupita ambapo wote wataanzia viwanja vya Jamhuri na kuishia katika viwanja hivyo.
 ”Vituo vya kuchukulia vifaa ni pamoja na Royal Village na Bunge jijini Dodoma huku kwa nje ya Dodoma kituo kitakuwa Mlimani City na kwamba vifaa vitatolewa kuanzia Juni 17 -23 mwaka huu.”amesema Kanali Bwigoge
Hata hivyo  amewataka wote walio jiandikisha kujitokeza kuchukua jezi hizo pamoja na kuongeza kuwa mbio hizo zitajumuisha makundi matatu, kilomita 5, 10 na 21.1.
Aidha amezitaja  zawadi za washindi ni kuwa  mbio ndefu mshindo wa kwanza ataondoka na kitita sh.1 milioni na kuanzia mshindo wa sita Hadi wa kumi watajinyakulia kiais Cha sh.100,000.ambapo kwa kilometa 10 mshindo wa kwanza atajinyakulia kitita Cha sh.500,000 huku mshindo wa sita Hadi wa kumi wakiondoka na shilingi 50,000.
 
Mkurugenzi wa Elimu,Utamaduni na Michezo JKT  Kanali Erasmus Bwigoge,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizindua  jezi pamoja na Vifaa vya Michezo vitakavyotumika katika Mbio za JKT Marathon 2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Elimu,Utamaduni na Michezo JKT  Kanali Erasmus Bwigoge ,akionyesha jezi pamoja na Vifaa vya Michezo vitakavyotumika katika Mbio za JKT Marathon 2023 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor