Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA MELI MPYA YA MV MWANZA MKOANI MWANZA.

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Hoteli ya NSSF kutoka kwa Meneja Usimamizi wa Miradi Eng. Helmes Pantaleo mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi huo Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kutoka ndani ya Meli Mpya ya Abiria na Mizigo ya MV Mwanza inayoendelea kujengwa katika bandari ya Mwanza South Mkoani Mwanza mara baada ya kagua maendeleo ya Ujenzi wa Meli hiyo tarehe 14 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mwanza mara baada ya kukagua Meli Mpya ya Abiria na Mizigo ya MV Mwanza inayoendelea kujengwa katika bandari ya Mwanza South Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.

Jengo la Hoteli itakayokuwa na hadhi ya Nyota tano ambayo inaendelea kujengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoani Mwanza.

Meli Mpya ya Abiria na Mizigo ya MV Mwanza inayoendelea kujengwa katika bandari ya Mwanza South.

About the author

mzalendoeditor