Featured Kitaifa

RAIS MAHAKAMA YA AFRIKA AFUNGUA KIKAO CHA MAJAJI WA MAHAKAMA HIYO JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud,akizungumza na waandishi wa habari   mara baada ya kufungua kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo leo Juni 14,2023  jijini Dodoma.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud, akiongoza  kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo kilichoanza leo Juni 14,2023  jijini Dodoma.Kushoto ni Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo, Modibo Sacko.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa   kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo kilichoanza leo Juni 14,2023  jijini Dodoma.Kushoto ni Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo, Modibo Sacko.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud,akizungumza na waandishi wa habari   mara baada ya kufungua kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo leo Juni 14,2023  jijini Dodoma.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud,akiwa katika picha ya pamoja na majaji baada ya kufungua kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo leo Juni 14,2023  jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud, amefungua kikao cha faragha cha Majaji wa Mahakama hiyo kinachofanyika jijini Dodoma kinacholenga kutathmini utendaji kazi.

Akizungumza baada ya kufungua kikao hicho, Jaji Aboud amesema Majaji hao ndio wanaotoa maamuzi ya mashauri mbalimbali na wamekutana ili kutathmini utendaji kazi wao kwa kuangalia maeneo waliyofanikiwa na yenye kero ili kutafuta ufumbuzi.

“Tunataka kuangalia utendaji wetu wa jumla kama tunakwenda sawa au tunatakiwa kujirekebisha ndio dhumuni kubwa la kikao hichi na kikao hiki ni cha pili, kile cha kwanza kilikuwa ni cha wataalamu wa masuala yanayohusu kazi yetu na kimeleta matokeo chanya na kimesaidia kuboresha utendaji kazi wetu,”amesema.

Amesema ndani ya miaka 16 nchi 34 zimeridhia kuanzishwa kwa mahakama hiyo na Afrika imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya haki za binadamu na watu kutokana na utayari wa nchi za Umoja wa Afrika.

“Hadi sasa tuna nchi 34 ambazo zimeridhia kuanzishwa kwa mahakama hii ikilinganishwa na huko nyuma, hivyo kwa kipindi cha miaka 16 angalau tumevuka nusu ya nchi hizo za Umoja wa Afrika ambazo ni 55, tungependa wanachama wote waridhie kwasababu ni chombo chao,”amesema.

Amesema kesi ambazo zimetolewa maamuzi ya msingi na maelekezo madogo katika mahakama hiyo ni 150 ambapo zaidi ya asilimia 50 zimetoka nchini Tanzania.

Naye, Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo, Modibo Sacko ameeleza kuwa wanashirikiana na nchi ya Tanzania kama nchi mwanachama ili kuhakikisha lengo la kuanzishwa kwake linatimia na kila nchi inapata inachohitaji kupitia mahakama hiyo.

About the author

mzalendoeditor