Featured Kitaifa

BREAKING NEWS:RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  amewateua wafuatao:- 

  1. i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). 
  2. ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa  Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi  wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki (CASSOA). 

Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila  ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu. 

iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu,  Wizara ya Maliasili na Utalii.  

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa  ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge na Uratibu); na 

  1. iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya  Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). 

Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023. 

About the author

mzalendoeditor