TIMU ya Al Ahly SC ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji Wydad Athletic Club waliokuwa pia wanashikilia taji hilo usiku wa jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Wydad walitangulia na bao la beki wake, Yahya Attiat-Allah El Idrissi dakika ya 27, kabla ya Mohamed Abdelmonem kuisawazishia Al Ahly dakika ya 78.
Al Ahly wanabeba Kombe kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kuwachapa Wydad 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Cairo na hilo linakuwa taji la 11 jumla kwao wakiendelea kuwa washindi wa mataji hayo mengi zaidi.