Featured Kitaifa

PUMA ENERGY YATOA GAWIO LA BILIONI 6.1 KWA SERIKALI , MSAJILI HAZINA ATOA NENO

Written by mzalendoeditor
SERIKALI imepokea hisa ya Gawio kutoka kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited kiasi cha shilingi Bilioni 6.1 kama sehemu ya wanahisa.
 
Akizungumza katika makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 leo Juni 8, 2023 jijini Dar es Salaam Msajili wa Hazina Bw.Nehemia Mchechu amepongeza hatua hiyo na kusema kwamba uhusiano ulioanzishwa na Kampuni ya Puma Energy, unapaswa kuungwa mkono na Serikali ya awamu ya 6 katika kudumisha sera ya kushirikiana na sekta binafsi.
 
Mchechu amesema kuwa ushirikiano huu, kama ambavyo Serikali inashirikiana na Puma Energy, unanufaisha pande zote mbili yaani Serikali na washirika wake wa sekta binafsi.
 
Pia ametoa rai kwa Bodi na menejimenti ya Puma Energy Tanzania kuendelea kuwa wabunifu wa huduma mbalimbali na kuona umuhimu wa kupanua shughuli za Puma Energy nje ya mkoa wa Dar es Salaam, akibainisha kuzidi kuwepo fursa kutokana na ukuaji wa miji mbalimbali sasa kwa kasi kubwa.
 
Aidha, Mchechu ameipongeza Kampuni ya Puma Energy kwa utendaji kazi wake uliotukuka hadi sasa na kupongeza jitihada za kampuni hiyo katika kuwekeza katika nishati mbadala hususani zilizoanzishwa hivi karibuni kama vile huduma za gesi ya LPG, matumizi ya nishati ya jua, na CNG
 
Akizungumza katika hafla hiyo mbele ya Msajili wa Hazina, Mkurungenzi Mtendaji-Puma Energy Tanzania Bi.Fatma Abdallah amesema kuwa Kampuni imeaza kuonyesha mwelekeo wa kufanya vizuri baada ya athari za kibiashara zilizosababishwa na COVID-19 na faida halisi kwa mwaka ulioishia Desemba 2022 iliongezeka kwa asilimia 11750 kutoka 2021
 
Amesema kuwa Puma Energy inamilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na asilimia 50 ya hisa za Kampuni
 
Bi.Fatma amethibitisha kuwa Puma Energy Tanzania iliripoti faida halisi ya TZS 24.4 bilioni (USD 10.32 milioni) kwa mwaka ulioishia Desemba 2022 na kwamba gawio lililolipwa kwa wanahisani kiasi cha shilingi 12.21 bilioni ( sawa na dola zaKimarekani milioni 5.15) ambayo ni 50 asilimia ya faida halisi ya Kampuni kwa mujibu wa Sera ya Gawio.
 
Mgao huo ulitangazwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Kampuni uliofanyika mei 10. 2023.
 
Kwa kuzingatia Sera ya Gawio, shilingi bilioni 7.3 ikiwa ni asilimia 30 ya faida halisi ya Kampuni kwa mwaka ulioishia Desemba 31. 2022 zitatengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Kampuni na shilingi Bilioni 4.88,ambazo ni asilimia 20 ya faida halisi ya kampuni. Zitahesabiwa kama mapato ya Kampuni.
 
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Puma Energy kanda ya Afrika, Fadi Mitri amesema Hundi za gawio zilizotolewa leo zinadhihirisha mchango chanya wa ushirikiano kati ya Puma Energy na Serikali ya Tanzania katika kusaidia ukuaji wa uchumi.
 
Amesema kuwa Puma Energy ina jukumu muhimu la kupeleka huduma za nishati sehemu mbalimbali nchini Tanzania sambamba na kusaidia jamii na Kwa kutumia mnyororo wetu wa kimataifa wa usambazaji,tumeweza kufanikisha usambazaji wa mafuta yetu yenye viwango vya juu vya ubora wakati wa changamoto ya hali ngumu ya soko la kimataifa.
 
Ameongeza kuwa suala lingine muhimu zaidi,faida iliyopatikana tumeigawanya sawa na watanzania kupitia malipo haya ya gawio kwa Serikali.
 
“Kuimarika kwa utendaji wa kampuni pia kunaiwezesha Puma Energy Tanzania kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya nishati ya Tanzania ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, huku pia ikisaidia jamii ya Tanzania.”Amesema
 
Nakuongeza kuwa “Mwezi huu tu tulitangaza mpango wa kuendeleza wahitimu kwa lengo la kuwapatia ujuzi vijana wa Kitanzania Zanzibar, wakati huohuo tukifanya uwekezaji katika mtandao wetu wa vituo vya mafuta vya rejareja na kuimarisha zaidi miundombinu ya vifaa vya kuhudumia usafari wa angakwa kuhakikishaTanzania inaongoza kwa kuwa na vifaa vya kisasa zaidi barani Afrika. Uwekezaji huu utaendelea na utasaidia kukuza uchumi wa Tanzania nzima.”
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Pumba Energy Dkt.Selemani Majige akimkabidhi Msajili wa Hazina Bw.Nehemia Mchechu mfano wa hundi ya shilingi Bilioni Sita na milioni mia moja (6,100,000,000/=) gawio kwa Serikari kama sehemu ya wanahisa. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam
 
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Pumba Energy Dkt.Selemani Majige akipokea hundi ya shilingi Bilioni Sita na milioni mia moja (6,100,000,000/=) kutoka kwa Mkuu wa Puma Energy Africa, Bw. Fadi Mitri. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina Bw.Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 kati ya Serikali pamoja na Kampuni ya Puma Energy iliyofanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Puma Energy Africa, Bw. Fadi Mitri akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 kati ya Serikali pamoja na Kampuni ya Puma Energy iliyofanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Pumba Energy Dkt.Selemani Majige akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 kati ya Serikali pamoja na Kampuni ya Puma Energy iliyofanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurungenzi Mtendaji-Puma Energy Tanzania Bi. Fatma Abdallah akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 kati ya Serikali pamoja na Kampuni ya Puma Energy iliyofanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina Bw.Nehemia Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Pumba Energy Dkt.Selemani Majige na Mkuu wa Puma Energy Africa, Bw. Fadi Mitri wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe bodi ya wakurugenzi Puma Energy Tanzania katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.1 kati ya Serikali pamoja na Kampuni ya Puma Energy iliyofanyika leo Juni 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
 
 
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
 
 

About the author

mzalendoeditor